"Eti simba, simba kitu gani?" Abdukiba, Kakake Alikiba amchokoza Diamond

Abdu Kiba aliachia maneno ya kumkejeli Diamond kwa jina lake la kimajazi – Simba

Muhtasari

• Matamshi haya yake hayakuchukuliwa kirahisi na baadhi ya mashabiki kindakindaki wa Diamond ambao walimjia juu.

Kakake Alikiba amtupia udongo Diamond Kwa jina lake la Simba
Kakake Alikiba amtupia udongo Diamond Kwa jina lake la Simba
Image: instagram

Msanii Abdu Kiba ambaye ni kaka wa toka nitoke kwa msanii Alikiba amezua gumzo kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuachia kauli moja kwenye Instagram yake akionesha kumtupia udongo msanii Diamond Platnumz.

Abdu Kiba aliachia maneno ya kumkejeli Diamond kwa jina lake la kimajazi – Simba, akisema kwamba simba si kitu kwani jina hilo halina sifa hata kidogo.

Kulingana na Abdu Kiba, jina Simba linakaa kawaida sana kwake kwa sababu simba analiwa, anazaa, anafugwa na hata anazaliwa. Kwa hiyo mnyama simba hana sifa yoyote ya kumfanya kuwa spesheli kando na zile hekaya na hadithi za kizamani kuwa ndiye mfalme wa msituni.

Eti SIMBA? SIMBA Sifa, SIMBA analiwa, SIMBA anafugwa 👑SIMBA anazaa, Bado anazaliwa✍🏿 @officialalikiba,” Abdu Kiba aliandika.

Matamshi haya yake hayakuchukuliwa kirahisi na baadhi ya mashabiki kindakindaki wa Diamond ambao walimjia juu na kumkunjia moja kwa moja pasi na kuyameza maneno yao.

Hatua ya Abdu Kiba pia kumtaja kakake Alikiba kwenye maneno hayo ilizua gumzo kali, kwani Alikiba na Diamond kwa muda mrefu wamekuwa wakijulikana kuwa watu mahasimu ambao hawawezi kupikwa kwenye chungu kimoja wakapikika.

“Acha uchoko, huweiz mfikia Simba Platnumz daima,” mmoja aliandika.

Dunia ya nyinyi kutafuta kiki kwa kumtukana Simba imeshapita nendeni na wakati ilo treni limeshayeya,” mwingine alishindwa kujizuia.