Tunafuata nyayo za Harmonize na Kajala, haki mapenzi wewe! - Stevo Simple Boy

Mrs Stivo Simple Boy alidokeza kuwa wapo njiani kuelekea ufukwe wa Diani kula bata.

Muhtasari

• Diani sisi hao tunakuja na mume wangu wa kipekee Stevo Simple Boy, hii itakuwa kama filamu - Gee aliandika.

Stevo simple boy asema wanafuata nyayo za wapenzi Harmonize na Kajala
Stevo simple boy asema wanafuata nyayo za wapenzi Harmonize na Kajala
Image: Instagram

Wapenzi wapya wanaotesa mitandaoni nchini Kenya Stevo Simple Boy na mrembo wake Gee wanazidi kuhanikiza katika janibu zote za mitandaoni, huku wakifika kiwango cha kujilinganisha na harmonize na meneja mpenzi wake Kajala Masanja.

Mpezni wa Simple Boy, Mrs Stivo Simple Boy alipakia picha wakiwa wamekumbatiana na kugandana kama ryba na kuachia ushauri kwa mashabiki wake kuwa furaha ni kitu cha kufanya uamuzi kuwa nacho.

Alidokeza kwamba pamoja na mpenzi wake mwanamuziki Stevo, wamo njiani kuelekea pwani ya Kenya kujivinjari katika maeneo ya ufukwe wa Diani.

“Furaha ni kitu cha kufanya uamuzi kumiliki, raha jipe mwenywe. Diani sisi hao tunakuja na mume wangu wa kipekee Stevo Simple Boy, hii itakuwa kama filamu,” Mrs Stevo Simple Boy aliandika.

Simple Boy ambaye anatesa mijini na kibao chake kipya cha harusi alifika kweney post ile na kuachia maoni yake huku akidokeza kwamba mahusiano yao sasa yanafaa kufananishwa na ya wachumba kutoka Tanzania, Harmonize na mwigizaji Fridah Kajala Masanja.

Mbona kufwata nyayo za @harmonize_tz na @kajalafrida 😂😂 mapenzi wewe,” Stevo Simple Boy aliandika kwa utani.

Stevo aliachia wimbo huo wa harusi wiki moja iliyopita huku wakionekana kushiriki katika kufunga pingu za maisha na Gee, tukio sawa na lile lililoonekana katika wimbo mpya wa Harmonize – Nitaubeba ambapo pia wanaonekana kufunga harusi pembezoni mwa bahari moja yenye madhari ya kutamanisha.