"Diana Marua yuko wapi? ako sawa?" Watu wamuuliza Yvette Obura, mama mtoto wa Bahati

Ni zaidi ya wiki tatu sasa ambapo msanii Diana Marua hajaonekana kwenye mitandao ya kijamii kama kawaida yake.

Muhtasari

• “Abeg, Mueni, najua huwezi kuweka siri sawa, plz tuambie kilichompata auntie Dee." mmoja aliuliza.

Yvette Obura aulizwa kuelezea kupotea kwa diana marua
Yvette Obura aulizwa kuelezea kupotea kwa diana marua
Image: instagram

Ni siku kadhaa sasa baada ya familia ya mwanamuziki Bahati Kioko na mkewe Diana Marua kupotea katika mitandao ya kijamii katika hali ambayo si ya kawaida.

Wiki chache zilizopita Marua alidokeza kuwa huwa anakumbwa na tatizo la kuchoka na hata kushindwa kifanya baadhi ya mambo kama kugeuka pindi anapokaribia siku za kujifungua.

Kilichowachanganya wengi ni baada ya kupakia ujumbe wenye maudhui meusi ya kupakia ndege aina ya njiwa huku akiachia ujumbe wenye ukakasi.

Tangu siku hiyo, Marua hajawahi kuonekana kweney mitandao ya kijamii tena kama ilivyokuwa kawaida yake na baadhi ya mashabiki wake wameingiwa na wasi wasi huku wakijaribu kumfikia mtu wa karibu nao kuwataarifu kinachoendelea katik maisha ya wanafamilia hao ambao si kawaida yao kupotea katika mitandao ya kijamii.

Bilas haka baada ya kufanya jitihada za kumfikia Marua bila mafanikio, mtu wa karibu ambaye sasa amejukumishwa na kujibu maswali ya uwepo wa Marua amekuwa ni mke mwenza ambaye ni mzazi mweza wa Bahati, Yvette Obura.

Obura ambaye ni mama mtoto kwa jina Mueni alipakia picha ya pamoja wakiwa na huyo binti wake na wengi waliofurika kweney upande wa kutoa maoni walikuwa wanataka kujua Diana Marua yuko wapi, iwapo kila kitu katika maisha yake kiko sawa na mbona amekuwa kimya kwenye mitandao yake ya kijamii yenye maelfu ya mashabiki.

“Abeg, Mueni, najua huwezi kuweka siri sawa, plz tuambie kilichompata auntie Dee. Kuonekana mrembo kama kawaida na mummy,” mmoja kwa jina Sharon Shine aliandika.

“Diana yuko wapi,” Charity Komora alisema.

“Yvette Obura mama Mueni, Diana Marua yupo sawa?” Njauzi alitaka kujua.