"Jay-Z na Beyonce wakujie mafunzo ya mapenzi halisi" -Willy Paul

Pozee alisema kuwa hivi karibuni atawapa mashabiki wake fursa ya kuwa mahakimu.

Muhtasari

• Pozee alisema atawapa mashabiki wake fursa ya kuwa mahakimu walichokuwa wakitayarisha yeye na Jovial.

• Alilinganisha mapenzi yao na yale ya Jay-Z na Beyonce.

Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Willy Paul na Jovial wadokeza kuwa kwenye mapenzi
Image: Instagram

Staa Willy Paul amekariri usemi wake wa hapo awali kuwa mapenzi yake na Jovial sio kiki na kwamba wako kwenye mapenzi ya ukweli.

Alisema kuwa yeye na Jovial wanawiana kwa hali na mali ikiwemo muziki na hilo ndilo linalowafanya wagande pamoja.

Willy Paul alisema siku ya Jumatatu kuwa yeye na Jovial waliyaweka mapenzi yao kwenye mizani na kuona kwamba wanaweza kukaa pamoja.

"Nilimwambia mpenzi wangu afungue roho na anieleze anachohisi kuhusu bwana mkunaji kwenye wimbo na pia yeye aliweza kunitathmini,"alisema.

Pozee alisema kuwa hivi karibuni atawapa mashabiki wake fursa ya kuwa mahakimu wa walichokuwa wakitayarisha yeye na Jovial kisha akalinganisha mapenzi yao na yale ya Jay-Z na Beyonce.

Aliongeza kuwa amekuwa akitaka kuwa kwenye mahusiano na mtu kama yeye, kuwa na mwanamuziki na msanii kama yeye na sasa aliweza kupata anayemfanana kwa mambo mengi.

"Beyonce na Jay-Z itabidi wamekujia mafunzo, nitazidi kuwaambia kuwa sio kiki, ni ukweli tunapendana,"alisema.

Hii ni baada ya mashabiki wake kuzungumzia uhusiano wake na Jovial na kudai kuwa ni kiki ya wimbo mpya ambao wanarekodi wawili hao.

Wiki hii wawili hao walianika mapenzi yao mitandaoni na wameonekana kuwa wenye mahaba sio kidogo.

" Mapenzi nayo ukipata Boss unasahau kila kitu walahi,"alisema mwanamuziki huyo.

Alipokuwa akimchumbia Jovial, Willy Paul alikuwa ameahidi kumpa Jovial furaha kwenye uhusiano wao iwapo Jovial angekubali kuwa mpenzi wake.

"@jovial_ke angalau kuwa na utu. Sikatai watu wanasema mimi ni bwana mkunaji, sijui ni kwa nini..kwa maisha lazima kila mtu anachoka na anaamua kutulia mimi hapa naomba nitulie na wewe. Nobody is perfect kwa hivyo usimhukumu mtu kulingana na mambo yake ya zamani.. Man is to error, ukinipa fursa hii ninakuahidi kukufanya uwe mwanamke mwenye furaha zaidi duniani,'Willy Paul aliandika.

Kabla ya uhusiano wao Jovial alikuwa amedai kuwa hawezi kuwa kwenye mahusiano na mwanamuziku huyo kwa sababu ana tabia za kitoto.