Wafahamu wanawake maarufu wanaopenda mtindo wa nywele fupi

Wanawake hawa kwa muda mrefu wamekuwa na mazoea ya kuteleza kwa mtindo wa kupendeza - kuachia nywele fupi.

Muhtasari

• Wanawake hawa waliamua kuwa na nywele fupi kwa sababu zao ambazo wengi wao hawajafichua ila wengine wao imeonekana kuwa ni asili yao ya urembo.

Image: Caroline Mbusa

Akili ni nywele ,kila mtu ana zake. Baadhi ya wanawake maarufu waliamua kutupilia mbali nywele ndefu wakiwa kwenye umaarufu wao na wengine wao kwenye muziki.

Wanawake hawa waliamua kuwa na nywele fupi kwa sababu zao ambazo wengi wao hawajafichua ila wengine wao imeonekana kuwa ni asili yao ya urembo.

Miongoni mwa hawa wana wake ni:

Nadia Mukami

Nadia mukami
Image: Nadia Mukami Instagram

Mwanamuziki huyo alikuwa na nywele ndefu kwa muda na alikuwa akionekana hadharani na nywele ndefu. Baada ya Nadia kupata ujauzito wake na kujifungua ndipo alipoamua kuzinyoa nywele zake na kutulia na nywele fupi mpaka sasa ila mara nyingine yeye hutumia wigi ama nywele bandia anapoenda kwenye shoo zake.

Femi One

Hitmaker huyu wa 'Utawezana' pia amekuwa akiweka nywele fupi kutoka hapo awali hata alipoanza muziki wake. Ingawa yeye hutumia wigi mara chache zaidi ,mwanamuziki huyu hupaka rangi za aina tofauti kwa nywele yake fupi.

Nana Owiti

Mkewe Kennedy Ombima almaarufu King Kaka pia amekuwa na nywele fupi kwa muda sasa ila pia yeye ako kwenye hiyo ligi ya kuiweka nyele yake rangi. Owiti ni mtangazaji wa kipindi cha Chatspot katika runinga ya Switch.

Wahu

Wahu
Image: Wahukagwi Instagram

Mwanamuziki Wahu Kagwi ameziweka nywele yake ikiwa fupi kwa muda mrefu sasa. Yeye huziweka nyele yake rangi za aina tofauti kwa wakati mwengine ila hatumii nywele bandia.

Pritty Vishy

Aliyekuwa mpenzi wake Simple Boy huwa ameeka nywele fupi ambayo huwa anaipamba kwa kuiweka rangi ama wakati mwingine yeye huvaa nywele bandia  ili kuwafurahisha mashabiki wake.

Vishy juzi baada ya kutangaza kuachana na msanii Madini Classic, anasherehekea kufikisha umri wa miaka 21 Jumatatu hii.

Rue Baby

Rue Baby
Image: Rue Baby Instagram

Mtoto wake mwanamuziki Akothee ambaye pia ni mwanamitindo, Rue baby huwa ameiweka nywele yake fupi kutoka kitambo. Mwanamitindo huyu huwa haiweki nywele yake rangi yoyote ila huwa anaiwacha ilivyo na rangi yale ya asili.

Huddah Monroe

Socialaiti,Huddah ameweka nywele fupi ila yeye hutumia nywele badia wakati mwengine.

Nyce Wanjeri

Mwigizaji huyu pia ni miongoni mwa wanawake maarufu wanaoweka nywele fupi.