Andrew Kibe: Bila Bien, hakuna Sauti Sol

Kibe alisema kuwa Bien ndiye aliye maarufu zaidi kuliko wenzake

Muhtasari

• Hii ni baada ya Apple Music kufichua sekta ya muziki wa Kenya ilivyodorora na kuwa nyimbo mbili tu ambazo ni za Bien ndizo zilizoangaziwa.

Image: Kibe na Bien

Mtumbuizaji Andrew Kibe almaarufu Kibe asema kuwa Bien ni mwanamuziki mkubwa bila bendi yake ya Sauti Sol.

Kibe alisema kuwa Bien ndiye aliye maarufu zaidi kuliko wenzake wengine wa bendi ya Sauti Sol na ndiye mwenye mafanikio zaidi ya wengine.

Alisema kuwa Bien anafahamu vyema jinsi ya kutoa wimbo utakaovuma na unaofaa na kuendelea kuwa mtu husika.

"Bila Bien hakuna Sauti Sol. Unapofikiria Sauti Sol, Bien ndiye atakayekuwa kwenye fikra zako wa kwanza ndipo hao wengine wafuate," alisema.

Kibe alisema pia kuwa Bien angekuwa mmmoja kati ya wasanii na watu maarufu wakubwa kwenye bara la Afrika.

Aliongeza kuwa madai ya Eric Omondi ya kusema kuwa Bien anaielewa sekta ya muziki kwa kuelewa showbiz ili kumtetea Bien na wakati huo huo kumfokea mwanamuziki huyo kwa kusema kwamba Bien anajua na kuelewa wanachotaka watu ila hataki watu wajue ni nini haswa.

Kibe alisema kuwa Eric Omondi hakukosea aliposema kuwa Bien anajua jinsi ya kuwa na mafanikio na kuwa ako na hiyo ya fomula.

"Bien anaweza kufanya kolabo ama kuimba na mtu yeyote na wimbo huo uvume. Hata mimi," alisema.

Hii ni baada ya Apple Music kuweka wazi jinsi sekta ya muziki wa Kenya ilivyodorora na kuwa nyimbo mbili tu ambazo ni za Bien ndizo zilizoangaziwa.

Nyimbo hizo mbili ni 'Inauma' na 'Dimensions' ambazo ziliimbwa na mwanamuziki huyo ndipo Eric Omondi akaongea na kuwakemea wanamuziki wa Kenya.

Eric Omondi alisema kuwa Bien anafanya kitu kilicho sahihi ila anadai kuwa mkubwa wa wasanii peke yake.

"Niliwaambia Bien ni wale watu ambao husoma usiku kama kila mtu amelala lakini mkiamka anawaambia mkacheze kandanda na yeye. Bien ni kitabu tuanchofaa kusoma ili kuelewa," Eric Omondi alisema.