"Bidii inalipa" - Betty Kyallo ashauri mashabiki wake

Mwanahabari huyo aliwasauri mashabiki wake huku akionekana kwenye mazingira ya kifahari kando ya gari ghali

Muhtasari

• Katika picha hiyo, Kyallo anaonekana kwenye jezi ya samawati ya timu ya Chelsea huku tabasamu lake likiwa limehanikiza.

Betty Kyallo akiwa anajivinjari
Betty Kyallo akiwa anajivinjari
Image: Instagram

Mwanahabari maarufu nchini Betty Kyallo amepakia picha yake maridadi akiwa anapunga upepo kando ya gari la kifahari lile la kufunguka paa.

Katika picha hiyo, Kyallo anaonekana kwenye jezi ya samawati ya timu ya Chelsea huku tabasamu lake likiwa limehanikiza katika pande zote na kuachia ujumbe wa kuwatia moyo wafuasi wake.

“Bidii na jitihada hulipa,” Betty Kyallo aliandika kwenye picha hiyo.

Katika picha ya pili, ilionesha jumba la kifahari kwa mbali ambapo taa za kufurahisha zilionekana kuwaka na magari kuegeshwa nje yake. Sehemu hiyo ilionekana kuwa ya burudani na kujivinjari.

Mashabiki wake walifurahia muonekano wake na kumsifu kwa kujiboresha hata baada ya kupitia changamoto nyingi katika mahusiano yake ya nyuma.

Mwingine aliutamani mwonekano wake wa kaptura fupi ambapo aliahidi kutia bidi maishani ili pia wakati mmoja akija kufanikiwa awe anavaa hivyo na wat uwasikuwe wanamhukumu kwa njia hasi.

“Nataka kutia bidii pia ndio ninunue gari na nikivaa kaptura fupi kama hiyo yako watu wasikuwe wananiita mtu wa kujiuza, Betty unaonekana wa moto sana kama kawaida yako,” Annitare Anne aliandika.

“Eiiyyy, hiyo jezi kwanza inaonekana kupendeza sana mwilini mwako,” mwingine kwa jina Its Omar alimsifia.

Kyallo amekuwa akitesa mitandaoni kwa picha zake nzuri katika madhari ya kifahari tangu kutangaza kusambaratika kwa mahusiano yake na wakili Nick Ndeda miezi kadhaa iliyopita.

Katika mahojiano na wanablogu, Kyallo alisema kwamba japo bado Imani yake katika ndoa haijafifia, lakini kwa sasa hayuko tayari kabisa kujaribu guu lake katika dimbwi la mapenzi na kusema angejipa muda zaidi ili kutathmini hali nzima kabla ya kufanya maamuzi yaliyotukuka.