Sina muda wa mwanamume mwingine-Akothee kwa mpenziwe

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa instaram alimwandikia na kumweleza mpenzi huyo jinsi anavyompenda sana.

Muhtasari
  • Alimwambia kuwa ana bahati sana kwani amempata akiwa tayari ameshamalizana na maisha yake na amefanya kila kitu katika maisha haya
Mwimbaji Akothee na mpenzi wake Bw Schweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii mmoja aliimba kuwa mpende akupendaye na asiye kupenda achana naye, lakini kwa msanii Akothee anaonekana kukolea kwa mahaba moto moto ya mpenziwe.

Wiki chache zilizopita, mwanamuziki huyo ​​alimtambulisha mpenzi wake mpya kwa Wakenya jambo ambalo liliwaacha wengi wakimpongeza kwa mafanikio hayo mapya.

Hii ilikuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani Nellyoaks ingawa hakushiriki sababu ya kuachana naye.

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa instaram alimwandikia na kumweleza mpenzi huyo  jinsi anavyompenda sana.

Alimwambia kuwa ana bahati sana kwani amempata akiwa tayari ameshamalizana na maisha yake na amefanya kila kitu katika maisha haya kwa uwajibikaji ambapo kukutana naye kilikuwa kitu pekee kilichobaki.

"Ni sisi tena, mpenzi unajua umenipata nikiwa nimemalizana na maisha ,nimefanya yote maishani mwangu na kwa kuwajibika sana, kitu pekee nilicho nacho. sikuwa nimefanya katika maisha yangu ilikuwa kukutana na wewe na kukupenda

Sasa tangu nilipokutana na wewe, nimekupa kila kitu, asali unachokiona ndicho unachokipata, mapenzi yangu kwako yanaongezeka kila siku,"Alisema Akothee.

Aliendelea na kumwambia kwamba hana macho wala wakati wa kuwa na mwanamume mwingine yeyote kwa sababu macho yake yana shughuli nyingi ya kumvutia.

Alimalizia kwa kusema kuwa anampenda, anamkubali, na kila wanapokuwa wawili tu huwa anafikiri anaota kwani bado haijampata kuwa yeye ni wake. Je, una maoni gani kuhusu wanandoa hao?

"Sina macho wala muda na mwanaume yeyote kwa sababu macho yangu yana kazi ya kukushangaa. I love you, admire you twin my, everytime tukiwa wawili tu mimi huwa NADHANI NINAOTA Bado haijanipata kuwa wewe ni wangu. MR OMONDI wangu nakupenda Deno."