Harmonize amtaka Ibraah kutoa ngoma baada ya nyingine, "Tumebaki wachache sasa!"

Wosia huu unakuja wiki moja baada ya wasanii Cheed na Killy kuondoka kwenye lebo ya Konde Gang.

Muhtasari

• Baada ya kuondoka kwa Cheed na killy, sasa Harmonize anabaki na wasanii Ibraah na Anjella ambao ndio walikwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kuwaandikisha mkataba.

Harmonize atoa ujumbe kwa Ibraah
Harmonize atoa ujumbe kwa Ibraah
Image: instagram

Wiki jana lebo ya Konde Music Worldwide ikiongozwa na mkurugenzi mkuu Harmonize waliwaaga wasanii Cheed na Killy ambao kwa taarifa zilizowekwa wazi ni kwamba mkataba wao ulikamilika.

Baadae kuliibuka na sekeseke kuwa wawili hao wameelekea katika bodi ya kusimamia Sanaa nchini Tanzania, BASATA kwa kile walimshtaki aliyekuwa bosi wao Harmonize kuwa aliikatisha mikataba yao kwa njia isiyo halali.

Katika taarifa na ambazo zilichapishwa na vyanzo vya habari, Cheed na Killy waliteta kuwa walipewa taarifa za kusitishwa mikataba yao kwa njia ya maneno hali ya kuwa waliingia mikataba na lebo ya Konde Gang kupitia kuandikiana.

Iliarifiwa kuwa Harmonize baada ya kutakiwa kujiwasilisha mbele ya BASATA ili kupata suluhu ila hakutokea yeye pamoja na uongozi wa lebo yake, katika kile ambacho sasa kimeonekana ni mzozo wa kisheria ambao wawili hao wameanzisha na Harmonize.

 Kwa upande wake, msanii Harmonize anaonekana kutotilia maanani maneno na madai ambayo wawili hao wameibua dhidi yake na badala yake ameelekeza macho katika wasanii wawili amabo alibaki nao, Ibraah na Anjella, na kuwataka kujitoa kwa nguvu kubwa kimuziki kwani sasa wamebaki wachache.

Akizungumzia hili kweney picha za Ibraah aliyepakia akiwa na tabasamu na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kuwa na tabasamu siku zote, Harmonize alimtaka kuachia ngoma baada ya ngoma kwani wamebaki wachache na kufanya kazi na timu ndogo ni rahisi kuliko awali wakiwa wengi.

CHINGA 🤴 Tumebaki Wachache Baba Ngoma JUU Ya Ngoma,” Harmonize alimwaambia.