Ujumbe wa mahaba wa Willis Raburu kwa mpenziwe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Katika ujumbe wake, Willis alieleza Namu kama mwanamke mkuu ambaye alileta amani si kwake tu bali kwa familia yake na marafiki pia.

Muhtasari
  • Willis na mpenzi wake Ivy wamebarikiwa na watoto wawili, huku wawili hao wakiwasherehekea watoto wao
Image: INSTAGRAM// IVY NAMU

Mtangazaji Willis Raburu ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wanafahamika sana mitandaoni kutokana na kazi yao na maisha yao binafsi

Willis na mpenzi wake Ivy wamebarikiwa na watoto wawili, huku wawili hao wakiwasherehekea watoto wao.

Huku akimlimbikizia sifa akisherehekea siku yakke ya kuzaliwa, Willis alimshukuru kwa kubadilisha maisha yake.

Katika ujumbe wake, Willis alieleza Namu kama mwanamke mkuu ambaye alileta amani si kwake tu bali kwa familia yake na marafiki pia.

Mtangazaji huyo wa runinga alisema anajivunia mchumba wake akibainisha kuwa hana chochote ila kumpenda.

“Namu wangu Tamu! Heri ya siku ya kuzaliwa nyota yangu! Mchumba wangu, Wewe ni moyo wa kweli, roho ya kweli na roho iliyotulia. Nuru yako huangaza hata nyakati za giza za dakika na unaleta amani na upendo mwingi kwangu na familia na marafiki zetu.

Ninajivunia wewe, ninakusherehekea na kumshukuru Mungu kwa ajili yako. Shine on! HAPPY BIRTHDAY! Ninakupenda sana," Willis aliandika.