Wahu afurahishwa kuona bintiye Nyakio akiwa amelala vizuri na mtoto wake mchanga

“Nilikimbia bafuni mara moja kurudi nikapata tukio hili hapa la kupendeza,” Wahu aliandika.

Muhtasari

• Wahu alipakia video hiyo na kusema kwamba ndio ya kipekee iliyomvutia jinsi dada hao walikuwa wamelala.

Wahu apakia video ya binti zake wakilala
Wahu apakia video ya binti zake wakilala
Image: Instagram

Mwanamuziki Wahu ni mama mwenye furaha baada ya kupokea binti yake wa tatu wiki moja iliyopita.

Wahu amezidi kuonesha upendo usiomithilika kwa mabinti wake kwenye mitandao ya kijamii, na Jumanne jioni alipakia klipu kwenye instastory yake ikionesha bintiye wa pili akiwa amelala na dada yao mgeni kwenye familia.

Katika video hiyo, Nyakio ambaye ni binti nambari mbili anaonekana amelala kando na dadake mchanga, Shiru huku wakiwa wamezama katika usingizi mzito, nyuso zao zikiwa zimeangaliana.

Wahu alipakia video hiyo na kusema kwamba ndio ya kipekee iliyomvutia jinsi dada hao walikuwa wamelala na kusema ni baada ya kuelekea bafuni muda mfupi na aliporudi ndio akapatana na ukio hilo la kuvutia.

“Nilikimbia bafuni mara moja kurudi nikapata tukio hili hapa la kupendeza,” Wahu aliandika.

Ikumbukwe msanii huyo pamoja na mumewe Nameless ambaye pia ni msanii wamekuwa wakijibizana na baadhi ya watu mitandaoni wenye dhana za kizamani kuhusu jinsia ya mtoto.

Mwishoni mwa wiki jana, Nameless alipakia picha ya kwanza akiwa amempakata bintiye Shiru na baadhi ya watumizi wa mitandao wakamtaka kufanya jitihada za kutafuta mtoto wa kiume, jambo ambalo aliwasuta vikali kwa kusema kwamba hizo ni mula za kizamani zilizopewa kisogo na majira ya nukta kuhusu jinsia.

Yeye alisema kwamba atafanya juu chini kuwahudumia mabinti zake na wala hatobabaishwa na wale wanaokwama kwenye mila na tamaduni za kizamani.