Diamond akoshwa na Mhindi aliyependezwa na Zuchu

Wimbo huo wa Zuchu ulimfurahisha Mhindi aliyemwonyesha Zuchu upendo.

Muhtasari

• Bosi huyo wa Zuchu alifurahishwa na wimbo huo uliyovuma hadi hadi kuwavutia Wahindi.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Mwanamuziki Diamond Platnumz amefurahishwa na Mhindi aliyependezwa na Zuchu.

Diamond alimwambia Zuchu jinsi alivyowafurahisha watu wengi kwa wimbo wake aliokuwa akiupigia debe wa Kwikwi wakiwemo Wahindi.

"Umemvuruga Mhindi wa watu huku @officialzuchu," Diamond alisema akiashiria kukoshwa.

Mhindi huyo alikuwa anamsifia Zuchu kwa wimbo wake mpya na kumwonyesha upendo huku akicheza wimbo huo.

Alisema kuwa anaupenda wimbo huo na kueleza jinsi mwanamuziki huyo wa WCB alivyomchanganya katika wimbo huo.

Mhindi huyo alionekana kuburudishwa na wimbo huo alipokuwa anapiga densi huku akiimba kwa furaha.

"Nampenda sana Zuchu, " Mhindi huyo alisema huku akikata maumbo kwa utamu wa wimbo huo wa Zuchu.

Jambo hilo halikutarajiwa kwani mwanamuziki huyo amekuwa akinunia mtu yeyote anayeonekana kumwonyesha Zuchu mapenzi .

Hivi majuzi, Diamond alishindwa kujizuia kuficha wivu baada ya Zuchu kumwonyesha staa wa Bongo Mbosso mapenzi kwa wimbo aliokuwa akipigia debe.

"Huyu hapa huyu nampendaaa🔥🔥" Zuchu aliandika maoni yake kwenye video hiyo.

Diamond hakuonekana kufurahishwa na ujumbe huo kisha baadaye kuuliza maswali ili ajue ni kwa nini Zuchu aliandika hilo.

Kwa utani Diamond aliuliza, "Yuko wapi?🤔"

Hata hivyo Diamond alikana kuwa kwenye uhusiano na Zuchu huku akidai kuwa mwanamuziki huyo ni msanii wake.

Alikana busu alilompa Zuchu wiki jana baada ya msanii huyo kumzawadi mkufu wa thamani na kusema kuwa hizo ni salamu za Kijerumani.