Ni wakati wa kupokea binti yangu - Diana Marua adokeza kujifungua

Diana amekuwa akidokeza kujifungua kwa muda wowote wiki hii

Muhtasari

• Mashabiki wameonyesha kuchoshwa na wapenzi hao wawili na kusema kuwa Marua alijifungua tayari.

Diana Marua

Mkewe mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati, Diana Marua ametangaza kuwa ako tayari kukutana na bintiye anayemtarajia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marua alipakia video iliyoonyesha akipelekwa hospitalini na mumewe.

Marua alikuwa ameashiria kuwa ulikuwa wakati wa kumpokea bintiye katika video hiyo iliyoonyeshwa akifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujifungua.

"Twende tumpokee malkia wetu," Marua alisema mtandaoni.

Hata hivyo, mashabiki wake wengine wameshuku hatua za rapa huyo na kusema kuwa anawachanganya watu.

Walisema kuwa mke huyo wa Bahati alishajifungua na kuwa video hizo anazopakia Diana ni za kitambo.

Baadhi ya maoni hayo ni kama:

@colletrolline - Ni kama Diana alijifungua mwezi mmoja uliopita.

@leen.wanjah - halafu anabadilisha tarehe kwa simu na anatuonyesha ili tusimshuku.

@leahchege789 - labda hata ni miezi miwili, tumewajua.

Hata hivyo, mashabiki wengine walimpongeza mama huyo kwa hatua hiyo kubwa ya kujifungua.

Hii ni baada ya Jumanne wiki hii wapenzi hao wawili kufichua jinsia ya mtoto wao kwa hafla ya kifahari.

Diana na Bahati walisema kuwa walikuwa wametarajia mtoto wa kiume ila wako tayari kumpokea na kumlea binti yao.

Mama huyo wa watoto wawili na mwengine mtarajiwa ameonekana kuwa na hamu ya kujifungua kwa jinsi ujauzito huo ulivyompiga vita.

"Nina furaha sana. Sina maneno. Wakati huu wote nimekuwa nikijua kuwa namtarajia mtoto wa kiume, kwa sababu ya alivyokuwa anageuka. Nilikuwa natumai kupata mtoto wa kiume baada ya hapo na nilikuwa tayari," Marua alisema akijizuia kulia.