Bahati awaacha wanamitandao njia panda kuhusu mkewe kujifungua

Bahati alipakia picha ya mkewe akiwa hospitalini na kuifuatisha na tarehe ya Jumanne Oktoba 25

Muhtasari

• Wengi walikisia Diana Marua kujifungua baada ya Bahati kupakia picha ya mkewe Instagram akiwa kando ya gari la wagonjwa.

Diana Marua

Watumizi wengi wa mtandao wamejiuliza maswali baada ya msanii Bahati kudokeza mke wake kujifungua.

Alipakia picha ya mkewe Instagram akiwa kando ambulensi huku akiwa ameshikilia tumbo lake jambo lililowafanya watumizi wa mtandao kuhoji iwapo ndo alikuwa anaelekea kujifungua.

"25.10.22, tafakari," Bahati aliandika.

"Hongera, tuko hapa tunangoja hadi pale atakapojifungua," kevin_musai1 aliandika.

"Namatakia heri njema anapoelekea kujifungua, nina hamu ya kumwona binti yenu. Huyo mtoto tutamlea pamoja na nyinyi kama vile tulifanya na hao wengine wawili," ukty_zam alisema.

"Haki jifungue tu, tumechoka na hii hadithi," winny_jerobon aliandika.

"Jamani, atazaliwa siku niliyozaliwa pia ," tandunikki alisema.

Baba huyo wa watoto watatu wa kuwazaa na mmoja wa kuasili amekuwa akiuliza watumizi wa mitandao ya kijamii kupendekeza jina ambalo atampatia mto wake mtarajiwa ambaye tayari ashafichua jinsia yake kuwa ya kike.

Kwa muda sasa staa huyo wa 'Barua Kwa Mama' amekuwa akidokeza kuwa mke wake angejifungua hivi karibuni ila baadhi ya wanamitandao wanaofuatilia sekeseke za familia yao wameonekana kutamaushwa na habari za Marua kujifungua mtoto wake wa tatu licha ya Bahati kudokeza kuwa amechoka na hata kuonyesha kuwa amevimba miguu.

Marua alikuwa amepakia picha iliyoonyesha akiwa hospitalini kisha kufuatisha na dokezo kuwa huenda kituo hicho cha hospitali kitakuwa makazi yake kwa siku kadhaa.

"Nyumbani mbali na nyumbani," Marua aliandika akionyesha uja uzito wake.

Takriban wiki mbili zilizopita, wanandoa hao walitangaza kutarajia mtoto wa kike katika tafrija ya kifahari ambayo Bahati aliandaa kwa njia ya kipekee kama kumbukumbu ya kumenzi bintiye mtarajiwa.