Mwanaume mzuri kuoana naye ni yule mamake amekufa - Huddah Monroe

Huddah alisema wanaume wanaojifanya watoto wa mama ni wagumu sana kutulia na mwanamke kwani mamake atakuwa anachukua muda wao mwingi.

Muhtasari

• Aliwashauri kina dada kukoma kuchumbiana na vijana ambao mama zao wanaishi peke yao kwa sababu watakuwa wanashindania muda wa kijana huyo.

Huddah awashauri kina dada kukaa mbali na wanaume watoto wa mama
Huddah awashauri kina dada kukaa mbali na wanaume watoto wa mama
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewacharukia wanaume ambao muda wote wanapenda kukaa karibu na mama zao na kusema kwamba wanaume kama hao ni vigumu sana kudumu kaika mahusino nao kwa mwanadada yeyote.

Kupitia mfululizo wa chapisho kwenye Instagram yake, Monroe alipakia video fulani ambayo ilisambazwa mitandaoni na staa wa Afropop kutoka Nigeria, Burna Boy akikumbatiana na mamake na kusema kwamba wanaume kama hao ni kibarua kigumu sana katika mahusiano.

“Huyu ni mwanaume mgumu sana kuchumbiana naye, wakati mama yake amemgandia hivi muda wote, basi sahau kabisa. Ndoa yenu haiwezi dumu,” Huddah Monroe aliandika kweney video ya Burna Boy na Mama yake wakikumbatiana kwa furaha.

Pia alizidi kusema kwamba aliwahi ambiwa na rafiki yake kuwa mwanaume bora wa kuchumbiana naye ni yule mamake amefariki ama yule ambaye muda wote yupo mbali sana na mama mzazi.

“Mmoja kati ya marafiki zangu ambaye ndoa yake ilivunjika aliniambia kuwa mwanaume wa Kiafrika mzuri wa kuoana naye ni yule ambaye mamake amefariki, au yule ambaye mamake ameolewa na yuko bize na mume wake. Wengine watakuwa wanashindana na wewe kwa kijana wake,” Huddah alielezea pasi na kubakisha maneno kwenye akiba.

“Na hakuna uongo hapo, wengi wa watoto wa mama ni bure sana kuchumbiana nao. Haswa wale ambao mama zao huishi peke yao. Usiharibu muda wako dadangu, kina mama kama hao wako pale mpaka mwisho wa Dahari. Kijana wake ataamua kutulia na mke wakati mamake amefariki au wakati amepata mume,” Huddah alizidi kusema.