Fahamu nyakati ambazo Diamond amekuwa akituhumiwa kuiba nyimbo

Wimbo'Yataniua' ulifutwa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia masuala ya hakimiliki.

Muhtasari

•Mbosso alimshirikisha Diamond katika wimbo wake 'Yataniua' ambapo ilidaiwa  walikopi maudhui ya wimbo 'Peace Be Unto You' wa Asake.

•Diamond pia alidaiwa kukopi wimbo wa H Baba wa 'Zilizopendwa' na 'Nataka Kulewa'  baada ya H Baba kulalamika kuhusu hayo.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Mwanamuziki Diamond amejipata kwenye chuma moto baada ya kudaiwa kuiba maudhui mbalimbali ya wasanii.

Hivi majuzi,Mbosso alimshirikisha Diamond katika wimbo wake mpya wa 'Yataniua' ambapo ilidaiwa kuwa walikuwa wamekopi maudhui ya wimbo 'Peace Be Unto You' wa mwanamuziki wa Nigeria, Asake, 

Wimbo huo ulifutwa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia masuala ya hakimiliki.

Zaidi ya hayo,Diamond alikopi pia muonekano wa mwimbaji huyo wa Afrobeats na kuibuka na mitikasi ya nywele yake.

Baadhi ya maudhui au mawazo mengine ambayo Diamond kukopi ni:-

Alidaiwa kuiba maudhui kutoka kwa wimbo wa mwanamuziki wa Namibia, King TeeDee kwenye wimbo wake 'The One' ambapo wananchi wa Namibia walimkemea .

Hata hivyo, TeeDee hakulalamika kuhusu suala hilo na alimpongeza Diamond kwa kuufanya wimbo huo kuwa bora zaidi, jambo lililowafanya mashabiki kushuku kuwa wasanii hao  walikuwa wamekubaliana.

Diamond pia alidaiwa kukopi wimbo wa H Baba wa 'Zilizopendwa' na 'Nataka Kulewa'  baada ya H Baba kulalamika kuhusu hayo.

"Wimbo wa Zilizopendwa ni wimbo wa H Baba. Mimi niliibiwa kazi yangu, kwa hivo nikae kimya? Kwa kusema kwangu ni kosa? Ama watu wanahisi namfuatilia ndio nifanikiwe... Nataka kulewa ulikuwa wangu nilipotaka kumshirikisha Q-chief aliuchukua akaimba, nikaseme,"  H baba alisema.

Wimbo wa tatu ambao Diamond alidaiwa kukopi ni wa mwanamuziki Otile Brown wa 'Such Kind Of Love'.

Diamond alikopi midundo ya wimbo huo na kutumia katika wimbo wake wa 'Naanzaje' .

Mnamo mwaka 2020, Diamond katika collabo yake na baby mama wake Tanasha Donna ya 'Gere' alidaiwa kukopi maudhui ya wimbo wa mwanamuziki wa Brazil, Iza wa 'Brisa'.