"Huna akili!" Paula amwambia Fahyma huku wakizidi kugombania penzi la Rayvanny

Paula alikuwa akikejeli kitendo cha Fahyma kupakia picha yake na Rayvanny

Muhtasari

• Fahyma alipakia picha akiwa na Rayvanny katika muonekano ulionuia kumchokoza Paula ambaye sasa amejibu vikali.

Fahyma, Rayvanny, Paula
Image: Instagram

Miezi michache iliyopita, mwanamuziki kutoka Tanznaia Rayvanny alidhibitisha kuachana na mpenzi wake tineja Paula Kajala katika kile alisema kuwa aliona mapenzi yao hayakuwa na uwuiano mzuri.

 

Baada ya kutengana, tetesi ziliibuka mitandaoni kuwa msanii huyo aliamua kurudi kwa mpenzi wake wa kwanza ambaye pia ni mama mtoto wake, Fahyvanny.

 

Japo Eayvanny hakulidhibitisha hilo, wengi walihisi wamerudiana na Fahyma baada ya kutengana miaka mitatu iliyopita.

 

Kwa muda sasa wanadada hao wawili, Paula Kajala na Fahyvanny wamekuwa wakitupiana michambo kwa njia fiche kupitia mitandao ya kijamii katika kile ambacho kimeonekana kuwa vita vya wivu wa mapenzi ya Rayvanny ambaye sasa yuko huru pasi na mpenzi yeyote baina ya hao wawili.

 

Kama ilivyoonekana kwenye chapisho la hivi majuzi lililopakiwa na Fahyma, alionesha video akiwa na Rayvanny na kwa kuangalia picha zake, lengo lake lilikuwa ni kumchokoza Paula ambaye anaonekana hajakubali kuvunjika kwa penzi lake na Rayvanny.

 

 Paula ambaye si mchache wa maneno Jumanne kupitia Snapchat yake aliachia chapisho la kujibu vikali kitendo hicho cha Fahyvanny huku akimwita mjinga ambaye anahitaji kupata akili ili kukoma kufanya vitu kama hivyo vya kupakia mwanaume – jambo ambalo alilitaja kama la kitoto na kipumbavu.

 

“Kama mpaka sasa kwa umri huo bado unapakia picha kwa status ili kumuumiza mtu, unahitaji elimu ya MEMKWA kwa sababu huna akili,” Paula alitupa bomu kwenye kambi ya jeshi la Fahyma.