Niite Mjaluo mtanashati, mwenye pesa - Willy Paul ajipiga kifua karibu na gari lake jipya

Wiki mbili zilizopita msanii huyo alinunua gari lake jipya aina ya Mercedes ambalo alisema ni kama kujizawidi kwa kutoa ngoma zenye maudhui safi.

Muhtasari

• Natumia hili la njano kwa sababu tumeshabihiana ushaelewa. Niite Mjaluo wa kupendeza mweney pesa zake nini na nini unajua - Willy Paul.

Willy Paul

Msanii Willy Paul amewanyamazisha wale wote waliokuwa wakifikiria gari aina ya Mercedes ambalo alisema amelinunua wiki mbili zilizopita si la kwake bali alikodisha.

Katika video moja ambayo aliipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul alionekana akiwa katika mavazi ya manjano, rangi sawa na gari hilo na kuwaambia wanamitandao kuwa pesa ni nzuri mtu unapokuwa nayo.

Katika muonekano huo ambao alisawasisha rangi ya nguo zake na gari lake, Pozee kama anavyojiita jina la kimajazi aliwaambia watu wamuite Mjaluo mwenye pesa na mapenzi kwa wingi kutokana na mtindo wake wa kipekee katika fasheni.

Alisema kuwa ana magari mengi san ahata alipata wakati mgumu kuchagua ni gari lipi ambalo angetoka nalo ila akaamua kulichagua hilo jipya la manjano kutokana na rangi yake kushabihiana na rangi ya nguo zake.

“Pesa ni nzuri, nilikuwa na wakati mgumu sana kuchagua ni gari lipi ningetoka nalo. Natumia hili la njano kwa sababu tumeshabihiana ushaelewa. Niite Mjaluo wa kupendeza mweney pesa zake nini na nini unajua..” Willy Paul alizungumza kwenye video hiyo kwa utani huku akilikaribia gari hilo.

Hivi majuzi aliposema amejitunuku gari hilo kama zawadi ya kufanya muziki mzuri wenye maudhui safi mwaka huu licha ya tuhuma za ubakaji kutoka kwa Diana Marua, wengi walidhani ni kiki za mitandaoni huku nambari ya usajili ya gari hilo ikizua mjadala mitandaoni.

Wengi walisema kuwa namba hiyo ambayo ilikuwa sita mara tatu inahusishwa na nguvu za kishirikina kutoka kwa jamii ya nguvu za gizani almaarufu Freemason na Iluminati.