Karen Nyamu apakia video ya mwanawe akimwimbia Samidoh heri njema za 'birthday'

Samidoh alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa Jumanne Novemba mosi.

Muhtasari

• Katika instastory hiyo, Nyamu na mwanawe mrembo walikuwa kwenye gari huku seneta huyo mteule akiwa amembeba mtoto wake wa kiume kwa upendo.

Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Image: Instagram

Wiki hii msanii Samidoh Muchoki anasherehekea siku yake ya kuzaliwa huku akiwa katika ziara ya muziki nchini Marekani.

Jumanne aipotangaza kwenye mitandao yake kuwa ni siku yake ya kuzaliwa, mastaa na watu mashuhuri mbalimbali walimsherehekea kwa kumtumia jumbe nzuri, akiwa katika jimbo la Boston, nchini Marekani.

Mmoja wa watu ambao hawakuachwa nyuma katika kumsherehekea ni mtoto wake ambaye wamezaa na mwanasiasa Karen Nyamu ambaye ni seneta maalum.

Kupitia video ambayo Nyamu alipakia kupitia instastory yake, mtoto huyo, Sam Michoki Jr alionekana akiwa ndani ya gari na kumuimbia babake wimbo wa kumtakia kheri njema akisherehekea kuzaliwa kwake.

Mtoto huyo aliwafurahisha wengi jinsi alivyokuwa akikariri maneno katika wimbo huo huku akiwa anatabasamu kutoka kona moja ya uso hadi nyingine.

"Awww heri njema ya kuzaliwa, baba Samidoh Muchoki," Nyamu alinukuu klipu hiyo ya kupendeza.

Katika instastory hiyo, Nyamu na mwanawe mrembo walikuwa kwenye gari huku seneta huyo mteule akiwa amembeba mtoto wake wa kiume kwa upendo.

Mvulana huyo alivaa tsheti ya machungwa huku akiketi kwa raha kwenye mapaja ya mama yake wakati wa kuendesha gari. Hakuweza kukazia macho yake ya kupendeza kwenye kamera ya simu huku akiimba kwa furaha wimbo wa siku ya kuzaliwa kwa baba yake mwenye, afisa wa polisi Samidoh.

Tabasamu lake la kuvutia na midomo yake nyororo ilihitimisha uzuri wake huku akimtakia babake siku njema ya kuzaliwa.

Msanii huyo alifichua jana kuwa ilikuwa siku yake mahususi, siku chache tu baada ya kumkumbuka marehemu mamake katika chapisho la kutia majonzi.

“Mwaka mwingine karibu na jua! Zaburi 25:5 Uniongoze katika kweli yako, na kunifundisha, kwa maana wewe ndiwe Mungu Mwokozi wangu, na tumaini langu liko kwako mchana kutwa. Kwa mwanamke aliyenizaa, Miriam, naona maombi yako yanatimia kila siku. Asante kwa kunipa uhai na kukuza talanta yangu katika umri mdogo. Baba, asante kutoka ndani ya moyo wangu. Mama yangu mlezi Seneta Betty M. Mama, wewe ni dira yangu, daima unanipa mwelekeo ninapoondoka, ishi Muda Mrefu,” Samidoh aliandika.