Eric Omondi ajibu madai ya Kibe ya kuwa anatafuta kiki kutumia muziki wa Kenya

Andrew Kibe alidai kuwa Omondi na Khaligraph walikuwa wanatafuta kiki kwa ugomvi wao

Muhtasari

• Katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema kuwa bado ataendelea kuwashinikiza wasanii kuwa na bidii katika kazi yao.

Kibe na Eric Omondi

Mchekeshaji Eric Omondi amejibu madai ya Andrew Kibe ya kuwa yeye kuwasuta wasanii ni jambo la kutafuta kiki,

Katika ukurasa wake wa Instagram, Omondi alisema kuwa bado ataendelea kuwashinikiza wasanii kuwa na bidii katika kazi yao.

"Mjadala umeanza na itabaki kuwa hivyo mpaka pale tutakapofanikiwa. HATUBANDUKI!" Omondi alisema.

Katika ukurasa wake wa YouTube, Andrew Kibe alizungumzia suala la Eric Omondi kuwazomea wanamuziki wa Kenya baada ya sherehe ya Oktoba Fest.

Alizungumza suala la mwanamuziki Khaligraph Jones kumkemea na kusema jinsi uvumi wake umekuwa ukididimia.

Kibe alisema kuwa kuna uwezekano wa kuwa Omondi na Jones walipanga jambo hilo la kukemeana mtandaoni.

"Eric Omondi bado ataendelea kuzungumza na anaongelesha Khaligraph Jones ila sina uhakika ikiwa huwa wamepanga kukemeana mtandaoni ili mdhani kuwa wana ugomvi," Kibe alisema.

Kibe alisema tukio la Eric Omondi kuenda bungeni kuhamasisha nyimbo za wanamuziki wa Kenya zichezwe ni kutafuta kiki.

Alisema kuwa suala hilo halitatui lolote kwenye sekta ya muziki wa Kenya ila alimpongeza kwa kugeuka gumzo mtandaoni kila wakati.

" Cheza nyimbo za Kenya kwa ukurasa wa YouTube wa nani? Nani atacheza nyimbo za Kenya maanake sio mimi. Huwezi kuniambia nicheze, una ukurasa wako na kila mtu ana kurasa zao za YouTube. Wewe cheza nyimbo hizo kama unataka kucheza,niambie unanilipa pesa ngapi kucheza nyimbo hizo ndipo tutazungumza," Kibe aliongeza.

Kibe alisema kuwa watu siku hizi hawatazami runinga na kuwa mambo sasa hivi yamekuwa ya mtandaoni kwa sana.