Nameless azungumza baada ya kudokeza kufanya upasuaji 'vasectomy'

Nameless alisema kuwa ilikuwa swali tu

Muhtasari

• Mume huyo wa Wahu alisema kuwa alikuwa anajaribu kuwapa watu moyo wa kuzungumzia suala hilo.

• Nameless alisema kuwa hata hivyo amekuwa akifikiria mbinu kadhaa za kpanga uzazi ila bado hajaamua haswa ni mbinu gani atatumia na kwa wakati upi.

nameless
nameless

Mwanamuziki Nameless amezungumza baada ya kudokeza kuwa anatafuta njia ya kuzuia uzazi ya Vasectomy.

Alikana madai ya kuwa alikuwa anatafuta mtaalamu wa kufanya upasuaji huo na kusema kuwa hataki kufanyiwa upasuaji huo.

"Mtoto wetu wa tatu anaedelea vyema, anafanana na Nyakio ila bado ni mapema kujua. Hilo chapisho lilikuwa swali tu ili kujua wanachofikiria watu kuhusu mambo ya kuzuia uzazi," Nameless alisema katika mahojiano yake na mwanahabari.

Mume huyo wa Wahu alisema kuwa alikuwa anajaribu kuwapa watu moyo wa kuzungumzia suala hilo.

Aliongeza kuwa mtoto alikuwa hajalala na alikuwa kwenye malezi wakati ambao alichapisha ujumbe huo katika ukurasa wake wa Facebook.

Alisema kuwa hata hivyo amekuwa akifikira mbinu kadhaa za kupanga uzazi ila bado hajaamua haswa ni mbinu gani atatumia na kwa wakati upi.

"Hata hivyo nilimaanisha kuwa ninaweza kutumia mbinu nyingine ila sikusema iapo ninapanga kufunga uzazi au kuzaa mtoto mwengine," Nameless alisema.

Baba huyo wa mabinti watatu alisema kuwa amekuwa akizungumza na mkewe suala hilo la kupanga uzazi.

Aliongeza kuwa amekuwa akifanya uchunguzi wake na pia kufanya majadiliano ili kuwa na uhakika wa atakachotumia.

"Bado Wahu hajasema lolote, anataka kujua mitazamo tofauti ya watu, na ana fikira wazi kuhusu jambo hilo. Hajasema kuwa ni lazima au sio lazima," mwimbaji huyo alisema.

Mwanamuziki huyo alitangaza kuwa anatafuta mtaalamu wa kufanya upasuaji huyo hivi majuzi, jambo lilomfanya kugeuka gumzo.

"Wueh 🥵... Ati mumesema mtu anaweza pata wapi vasectomist mzuri😅😅😅😅🥴...#BabaGalzzzzzzz😴😴😴," Nameless aliandika.