Huku inje wanawake si wazuri sana wamebeba kamdudu-Ushauri wa Pritty Vishy

Katika chapisho mwanasosholaiti huyo alikuwa na mashauri machache kwa wanawake walioolewa.

Muhtasari
  • Aliendelea kueleza kwamba wanaume wasio waaminifu hawatabadilika kamwe au kuacha tabia zao
  • Alidokeza kuwa ni bora kwa mwanamume kuwa na mke wa pili kuliko kudanganya
Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Pritty Vish Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Image: Facebook

Mwanaosholaiti Pritty Vishy ambaye pia ni mpenzi wa zamani wa rapa maarufu Stivo Simple Boy amechapisha ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii uliowaacha wanamitandao na gumzo.

Katika chapisho mwanasosholaiti huyo alikuwa na mashauri machache kwa wanawake walioolewa.

Pritty Vishy aliwashauri wanawake walioolewa wasiwafurahishe waume wanaodanganya.

Aliendelea kueleza kwamba wanaume wasio waaminifu hawatabadilika kamwe au kuacha tabia zao.

Alidokeza kuwa ni bora kwa mwanamume kuwa na mke wa pili kuliko kudanganya.

Kulingana na Pritty Vishy, ​​kuna wanawake wengi ambao wanatafuta  wanaume wao na wanaweza kupata ugonjwa  wakati wa kudanganya.

"Ushauri wangu kwa wanawake, usikubali mwanamume mdanganyifu..kwa sbabu atafanya hivo tena na tena.badala yake msaidie kutafuta mke wa pili, huku inje wanawake si wazuri sana wamebeba kamdudu."

Pritty aliendelea kunukuu Biblia akitaja kwamba kudanganya kunabadili wanaume.

"Na kumbuka biblia inasema lakini sijui ni kitabu gani..unapolala na mwizi pia nawe unakuwa mwizi maana wanabadilishana roho alafu Ana rudi kulala na ww heeeeh ...I might be young and not Married bt NOTE."

Alimalizia kwa kusema kwamba huenda hajaolewa lakini ilikuwa muhimu kwa wanawake kuzingatia ushauri wake.