"Kwenda huko, sikutaki" Pritty Vishy asema baada ya Owen kumkataa

Vishy kwa hasira alisema kwamba msanii Owen ana mahitaji mengi kwa mwanamke mmoja.

Muhtasari

• Daddy Owen alisema kuwa anataka kuoa msichana wa kijijini ndipo Pritty Vishy akatuma ujumbe kuwa anataka kuwa mke wake

• Vishy alisema kuwa amekata tamaa na kuwa hataki tena kuwa mke wa Owen kwa kuwa na mahitaji mengi.

Aliyekuwa mpenzi wa Simple Boy, Pritty Vishy amesema kuwa hamtaki tena mwimbaji wa nyimbo za injili Daddy Owen.

Vishy alijieleza na kusema kuwa Daddy Owen ana mahitaji mengi ya mke anayehitaji ambapo hamna wanawake wengi wenye mahitaji kama hayo.

Katika mahojiano yake na mwanahabari, Vishy alisema kuwa Daddy Owen anafaa kuwaelewa wanadada wa kisasa.

“Nilikuwa namtaka lakini sasa ni kama atavuka upande wa Uganda, ni mwanaume yupi ambaye anataka kuwa na ufisadi? Nasikia hataki mwanamke ambaye yuko kwenye mtandao wa TikTok na anayeongea Kizungu kingi,” Vishy alisema.

Aliongeza kuwa yeye ni mwanamke anayeongea Kizungu cha Uingereza na hicho hakiwezi kikabadilika kwa sababu ya Owen.

Alisema kuwa Daddy Owen atafute kwengine kwa kuwa huku Kenya wanawake hata wale ‘kienyeji’ ambao Owen anataka wako kwenye mitandao siku hizi.

“Hata Tanzania siku hizi wanajaribu kizungu na kuwa kwenye TikTok,” alisema.

Mwanavlogu huyo alisema kuwa ana sifa anazohitaji Owen kwa mwanamke ikiwemo rangi ya weusi na kusema kuwa ‘filter’ za mtandaoni zisiwadangaye watu.

Aliongeza kuwa hata wanawake ambao wako kwenye mitandao ni wacha Mungu na wanapenda maombi.

Vishy alidai kuwa Owen anadanganya suala lake la kupata ombi la wanawake zaidi ya elfu kwenye Instagram wakitaka kuwa wake wake.

“Sijafurahishwa na jambo hilo, kwani wewe ni nani useme kuwa umepata jumbe zaidi ya elfu kutoka kwa wanawake wakitaka kuolewa na wewe?” Vishy alisema.

Hivi majuzi, Vishy alikuwa amewatuma mashabiki wake wa Instagram kumwambia mwimbaji huyo kwa ana sifa za kuwa mke wake na anataka kuwa mke qwake.

Alijitambua kuwa ‘kienyeji’ na hata mcha Mungu.