Sitaleta mtoto hii dunia-Muunda maudhui Eve Mungai awajibu wakosoaji wake

Aliteta kuwa wale wanaomshinikiza apate mtoto hawatashiriki majukumu ya kumtunza mtoto.

Muhtasari
  • Shinikizo hilo linaonekana kumsukuma MwanaYouTube huyo na hatimaye ameamua kushughulikia mada hiyo tena
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Mungai Eve

Mtayarishaji wa maudhui nchini  Eve Mungai ametoa kauli ya uchungu kujibu shinikizo linalozidi kumtaka apate mimba.

Shinikizo hilo linaonekana kumsukuma MwanaYouTube huyo na hatimaye ameamua kushughulikia mada hiyo tena.

Katika taarifa ya ambayo alitoa kwa mashabiki wake mitandaoni, Eve Mungai alisema kwa ukali kwamba hatakubali shinikizo la mitandao ya kijamii.

Alibainisha kuwa hawezi kupata mtoto kwa sababu tu mashabiki wake walikuwa wakimshinikiza.

Aliendelea kusema kwamba ataishi maisha yake na kufurahia kila sehemu yake.

Aliteta kuwa wale wanaomshinikiza apate mtoto hawatashiriki majukumu ya kumtunza mtoto.

Kwa hivyo anaamini ni uamuzi wake na sio wa umma wakati anapaswa kupata ujauzito.

"Jambo moja kunihusu,sitaleta mtoto hii dunia juu ya shinikizo ya mitandoa ya kijamii!!nitaishi maisha yangu na kufurahia kila sekunde na kufanya kile nataka,Kama unasubiria Eve azae juu ya wambea kama watalisha mtoto wangu wewe mtangoja!" Ujumbe wa Mungai ulisomeka.