Arrow Bwoy amsherehekea mpenziwe Nadia Mukami akifikisha miaka 23

Wawili hao wana mtoto mmoja pamoja ambaye ni wa kiume kwa jina Kai.

Muhtasari

• Mama wa ajabu kwa mwana wetu, mpenzi wa ajabu na rafiki , @nadia_mukami Nampenda mwanamke ambaye umekuwa - Arrow Bwoy aliandika.

Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bwoy
Nadia Mukami na mpenzi wake Arrow Bwoy
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya huku nchini Arrow Bwoy mwenye asili ya Uganda amemsherehekea mpenzi wake Nadia Mkuami huku akifikisha miaka 23 Jumatano Novemba 9.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Arrow Bwoy alimmiminia sifa na kumvisha koja la maua Mukami kwa kusema kwamab kila sekunde iendayo kwa Mungu anazidi kupenda jinsi mwanamke huyo anazidi kua.

Mkali huyo wa Dodo alifichulia mashabiki na watumizi wa mitandao kuwa ukaribu baina yake na Mukami kila siku unazidi kukua na anazidi kupendwa mwanamke anayekua katika Nadia Mukami.

"Ukaribu wetu unazidi Kuimarika Kila Siku. Mama wa ajabu kwa mwana wetu, mpenzi wa ajabu na rafiki , @nadia_mukami Nampenda mwanamke ambaye umekuwa ... Mwenyezi akujalie Kila la heri unapofikisha miaka 23 😁 heri njema ya kuzaliwa malkia wangu nakupenda," Arrow Bwoy alisema.

Pia alitilia utani kwenye maneno yake akimtakia Mukami kupona haraka kutokana na kuzaa ili tena waweze kushiriki mapenzi.

Ikumbukwe Nadia Mukami na Arrow Bwoy wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu ambapo mapema mwaka huu walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza waliyempa jina Kai.

Mukami alimsherehekea Kai mwezi mmoja uliopita alipokuwa akifikisha miezi sita tangu kuzaliwa kwa ujumbe mtamu huku akisema kwamba mtoto huyo ndiye aliyemheshimisha na kumhamishia anwani ya jina lake kutoka kuitwa msichana hadi kuitwa mama mwafulani.