Madini Classic ashirikiana na Classton Vital kwenye wimbo 'Shaku Shaku'

Wawili hao wameahidi mashabiki wao miradi zaidi katika siku zijazo

Muhtasari

•Wimbo huo ni mchanganyiko wa Bongo ambao ni wa kumsifia mwanamke anayefahamika kwa jina  'Amina'.

Msanii Madini Classic na mchumba wake Pritty Vishy katika hafla moja awali
Msanii Madini Classic na mchumba wake Pritty Vishy katika hafla moja awali
Image: Instagram

Madini Classic ameshirikiana na Classton Vital katika wimbo wake mpya wa  'Shaku Shaku'. Wimbo huo ni mchanganyiko wa Bongo ambao ni wa kumsifia mwanamke anayefahamika kwa jina  'Amina'.

Classton ni mtunzi wa nyimbo, mtaalamu wa mitindo na mwanamuziki.

Madini alianza kazi yake ya muziki akiwa Tanzania kabla ya kuhamia Kenya kisha baadaye kuelekea pwani.

Madini anavutiwa sana na muziki wa Bongo ambao alikuwa akiimba kabla ya kuwa maarufu, na hili linaelezea mtindo anaopenda wa kimuziki.

Alivuma zaidi kwa mara yake ya kwanza mwaka wa 2017 na tangu wakati huo amekuwa akijitahidi mno katika kazi yake. Kwake anga ndio kikomo.

Miongoni mwa nyimbo zake maarufu ni 'Bingo Bango' ambao alimshirikisha baby mama wa Mulamwah, Carrol Sonnie kama video vixen.

Pia ana wimbo unaoitwa 'Forever' ambao amemshirikisha Pritty Vishy kama vixen.

Je, 'kibao Shaku Shaku' kimeweza ama?