Mpenziwe Eric Omondi, Lynne azungumzia kupoteza mimba yake

Omondi alitangaza kuwa Lynne alipoteza ujauzito wake jana Jumanne

Muhtasari

β€’ Katika ukurasa wake wa Instagram, Lynne alisema kuwa hakuamini tukio hilo lingetendeka.

Eric Omondi na Lynne

Mpenziwe Eric Omondi, Lynne ameandika ujumbe wa  kuhuzunisha kwa mwanawe baada ya kupoteza mimba aliokuwa nayo. 

Katika ukurasa wake wa Instagram, Lynne alisema kuwa hakuamini tukio hilo lingetendeka.

"Kwa malaika wangu. Siwezi amini kuwa umeenda. Ninashukuru ulikuwa ndani yangu kwa wiki nane. Ninaomba msamaha kwa kuwa sitaweza kuona uso wako mzuri au kukanda miguu yako midogo. Nitakupenda milele," Lynne aliandika.

Mashabiki wake wakiwemo watu maarufu walimfariji mama huyo.

"Yote yatakuwa sawa, tunakuombea ," Pierramakenaofficial alisema.

"Upendo zaidi kwako, Mungu akupe amani na Eric kwa wakati huu wa majaribio," myhairmypride aliandika.

 Eric Omondi ndiye aliwafahamisha watu mtandaoni kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo,kupitia Instastory zake, Omondi bado aliwajulisha watu jinsi Lyyne anavyondelea baada ya kumpoteza mwanawe.

Alipakia video alipomtembelea Lynne hospitalini kisha akasema kuwa anaendelea vyema .

Hata hivyo, mchekeshaji huyo alikuwa mwenye huzuni alipokuwa anamsaidia mpenzi wake wakiwa hospitalini.

Kama Lynne, Omondi pia alikuwa amemwandikia mwanawe ujumbe.

"Jana usiku ulikuwa usiku mrefu maishani mwanguπŸ˜₯πŸ˜₯. Tulijitahidi kwa zaidi ya saa tano ili kujaribu kumwokoa malaika wetu mdogo ila Mungu alikuwa na mipango mingine. Hatukukutana nawe ila tulikuhisi na kuwa na kumbukumbu zako na tutazidi kukupenda milele πŸ•ŠπŸ•ŠπŸ•―πŸ•―. Heshima kwa wanawake wote, hakuna mwanamume duniani mwenye nguvu kama hiyo. @l.y.nn.e kuwa na nguvu.. Yote yatakuwa shwari....," Omondi aliandika.