Bahati afurahia muda mzuri na binti yake na 'babymama' Yvette Obura, Mueni

Msanii huyo alionekana akitembea na binti yake huyo huku akimmiminia sifa na kumvisha koja la maua kwa maneno mazuri.

Muhtasari

• Mueni ndiye binti pekee Bahati alibarikiwa naye akiwa na mahusiano na mwanadada Yvette Obura kabla ya kutengana.

Bahati na bintiye Mueni
Bahati na bintiye Mueni
Image: Instagram//Bahati

Msanii Ommy Dimpoz siku fulani nyuma wakati wa sakata lake na babake, aliwahi shauri wanamitandao kuwa kitu chenye ubora wa aina yake ambacho mzazi anaweza kumpa mwanawe basi ni mapenzi, na uwepo katika maisha ya mtoto.

Msanii Bahati Kioko amewafurahisha wengi baada ya kumuandikia ujumbe bintiye kifungua mimba kutoka kwa mzazi mwenziwe Yvette Obura, Mueni Bahati huku akimuahidi kusimama naye katika muda wote wa maisha yake.

Bahati alimwambia bintiye kuwa muda wote akakuwa shabiki wa kazi zake za kimaisha namba moja na pia kumpa mapenzi yote ambayo mtoto anaweza akahitaji kutoka kwa baba mzazi.

“Kwako Binti Yangu wa Kwanza- Kuzaliwa. Nitakuwa hapa kwa ajili yako kila wakati. Daima nitakuwa Shabiki wako Mkuu. Nakupenda kwa moyo Wangu wote @Mueni_Bahati,” Bahati alimmiminia sifa bintiye.

Katika picha hiyo ambapo aliipakia Instagram, Bahati alionekana kutembea na bintiye Muneni huku wameshikana mikono wakicheka na kutabasamu kwa furaha.

Mueni ndiye binti pekee Bahati alibarikiwa naye akiwa na mahusiano na mwanadada Yvette Obura kabla ya kutengana na msanii huyo uamua kumuoa mwanablogu wa YouTube, Diana Marua.

Pamoja na Marua, wamebarikiwa na watoto watatu, wa kiume mmoja na wasichana wawili.

Bahati na Diana wiki mbili zilizopita walitangaza kumpokea mtoto wao Malaika baada ya muda mrefu mashabiki wao kusubiria habari hizo tangu walipotangaza kuenda leba kwa ajili ya maandalizi ya kumpokea mtoto huyo.

Kando na watoto hao na Diana, pia msanii Bahati alikuwa na mtoto mmoja wa kuasili kwa jina Morgan ambaye alimuasili kutoka mitaani kama njia moja ya kurudisha mkono kwenye jamii kwani yeye pia alikuwa ni mtoto wa mitaani baada ya kuachwa yatima akiwa katika umri mdogo zaidi.