Sitawasikitisha tena-Wavinya awahakikishia Wakenya baada ya kumkejeli

Bosi huyo wa Kaunti ya Machakos ameahidi kwamba hataonekana tena akiwa mcheshi jinsi alivyokuwa siku chache zilizopita.

Muhtasari
  • Amebainisha kuwa Wakenya wanapendelea kumuona akiwa amependeza na si vinginevyo, na kuongeza kuwa hatakatisha tamaa matarajio yao
GAVANA WA MACHAKOS WAVINYA NDETI
Image: TWITTER

Gavana Wavinya Ndeti ameshiriki  picha nzuri ili kuwathibitishia Wakenya kwamba kabati lake la nguo limepangwa vizuri baada ya Wakenya kumdhihaki kwa kuonekana mcheshi.

Bosi huyo wa Kaunti ya Machakos ameahidi kwamba hataonekana tena akiwa mcheshi jinsi alivyokuwa siku chache zilizopita.

Amebainisha kuwa Wakenya wanapendelea kumuona akiwa amependeza na si vinginevyo, na kuongeza kuwa hatakatisha tamaa matarajio yao.

Pia aliwaambia Wakenya kwamba anawapenda,licha yao kumkejeli kwa ajili ya mavazi yake.

"Lakini nyinyi wakenya, enyewe mmeniweza. Jambo moja najua sasa unanipenda kuwa smart... Sitadissapoint tena. Siku hizi najali zaidi mahitaji yako. Love you guys," alisema.

Siku chache zilizopita,gavana huyo alionekana hadharani na mavazi ambayo hayakuvutia wengi.

Kulingana na Wakenya ambao walimdhihaki bosi huyo wa kaunti kulingana na mwonekano wake wa mavazi,alionekana kama mwanamke wa kijijini ambaye hanaada mtindo wa kisasa wa mavazi.