Mwimbaji Ruth Matete azungumzia vifo vyenye utata katika familia

Ruth Matete alikuwa anawaza jinsi watu katika familia yake wamewapoteza wapenzi wao

Muhtasari

• Matete alisema amekuwa akiishi mjini baada ya kuhamishwa na baba yake kutoka kijijini ambapo alikuwa anaishi na mama yake.

•Matete alisema kuwa mumewe hakuwa na matumaini ya kupona au kuendelea kuwa hai baada ya kupata ajal

Ruth Matete
Image: Ruth Matete Instagram

Mwimbaji wa yimbo za injili, Ruth Matete amefunguka kuhusu matukio tatanishi ya vifo katika familia yake.

Kwenye Instagram, Matete alisema ameshangazwa na matukio ya vifo katika familia yake kwa jinsi yanavyofanana. 

"Mama yangu alifariki nilipokuwa na umri wa miaka 8. Baba yangu wa kambo alimpiga sana na akapelekwa hospitali akiwa na majeraha. Nilikuwa bado nikiishi naye na baba yangu wa kambo. Kwa hiyo, mama yangu alipogundua kwamba huenda asifanikiwe, alimpigia simu baba yangu na kumwomba aje kunichukua," alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema amekuwa akiishi mjini baada ya kuhamishwa na baba yake kutoka kijijini ambapo alikuwa anaishi na mama yake.

Alifichua kuwa wazazi wake walimzaa nje ya ndoa kisha baadaye wote wawili wakajitosa kwenye ndoa tofauti. 

"Mama yangu alifariki miezi michache baada ya mimi kuja Nairobi. Baba yangu alioa mwanamke mwingine hapa Nairobi ambaye pia alifariki baadaye. Baba yangu wa kambo alifariki mwaka uliopita," aliandika.

Mwimbaji huyo pia alizungumzia kifo cha mumewe ambacho kulingana naye, hakikuwa cha  kawaida na kukihusisha na matukio ya wanafamilia wake kupoteza wachumba.

Matete alisema kuwa mumewe hakuwa na matumaini ya kupona au kuendelea kuwa hai baada ya kupata ajali na hadi alichukua hatua ya kumweleza hayo ila hakutilia maanani  alichokuwa akiambiwa.

"Aliniambia yote aliyotaka nifanye (nilihisi kuwa ni zile sinema za Afro). Alinipa jina la mtoto bila kujali jinsia. Toluwa ni jina la jinsia zote. Alinipa ujumbe kwa dada yake na kaka yake pia.Mungu alimpa wiki mbili. Katika majuma hayo mawili, kila nilipoenda kumtembelea, aliniuliza “Oh! Bado niko hapa? "

Ni kama alikuwa anasubiri kifo. Nilihisi kama hakupigania kuishi. Lakini hata hivyo, sitawahi kujua kikamilifu," Matete alisema.

Aliwaomba watu kumwombea yeye na familia yake na hata kuwashukuru waliokuwa wakimwombea katika msiba wake.