Daddy Owen adokeza kupata kidosho wa kumpa mapenzi

Daddy Owen alipakia video ya mwanadada wa kijijini akisakata densi

Muhtasari

• "Nimeambiwa niwache kuwasumbua watu kwa kuwa wasichana wote wa kijijini 'vienyeji' wamebaki wako TikTok saa hii.

• "Lakini huyu ana mitindo ya densi wueh," Owen aliandika.

Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Msanii tajika wa nyimbo za Injili, Daddy Owen amedokeza kupendezwa na mwanadada mmoja wa mashambani.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, alipakia video ya msichana huyo akisakata densi kwenye TikTok.

Alisema kuwa kuna uwezekano kuwa harakati zake za kutafuta msichana  kienyeji kuoa zimefika mwisho.

"Nimeambiwa niwache kuwasumbua watu kwa kuwa wasichana wote wa kijijini 'vienyeji' wamebaki wako TikTok saa hii. Lakini huyu ana mitindo ya densi wueh," Owen aliandika.

Dady Owen alikuwa amesema msukumo wake wa kutaka kuoa msichana wa kijijini kuwa uhusiano wa rais William Ruto na mkewe Rachel Ruto ambao ulianza zamani hadi sasa hivi.

"Nataka mwanamke kienyeji mweusi kabisa, mcha mungu, wa kijijini kabisa," alisema katika mahojiano na stesheni moja ya  redio ya humu nchini.

Daddy Owen aliweka wazi kuwa hataki msichana wa mjini akidai kuwa wasichana wa mjini mara nyingi huwa wajuaji sana.

Alisema yuko tayari kumfundisha mke wake kutoka kijijini na kumweka sawa asije akachepuka akionja maisha mjini.

"Awe katika miaka ya 20 au 30," alisema.

Kwenye mtandao wa Instagram, Owen alidokeza kuwa baadhi ya wanadada Wakenya tayari wameanza kujipendekeza kwake.

"Nilisema mwanamke mweusi, watu wanakuja inbox na ati melanin.. ukishasema melanini wewe si kienyeji," alisema.

Katika mahojiano ya awali na Word Is, Owen alifichua hofu yake kwamba umri wake unasonga na bado hajapata familia yake.