Eric Omondi amkejeli mwanawe Museveni kwa video, kwa kusema kuwa atateka Nairobi

Omondi aliashiria kuwa Muhoozi atachanganyikiwa iwapo angejaribu kuteka Nairobi

Muhtasari

• Video hiyo ilionyesha Omondi (akimwigiza Muhoozi) akijitokeza kwa helikopta akiwa amevalia mavazi kamili za kijeshi, akarukia Kenya.

• Eric na  maafisa waliovalia kijeshi wakitazama huku na huku kwa mshangao huku wakionekana kuchanganyikiwa kuhusu mahali walipotua.

Eric Omondi na wenzake wakimwigiza Muhoozi
Image: Eric Omondi Instagram

Mchekeshaji Eric Omondi amemkejeli mwanawe Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuhusu suala lake la kuvaamia Kenya.

Omondi alimkejeli Jenerali huyo kwa video ya kuchekesha aliyopakia kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter.

Ujumbe aliokuwa akijaribu kupitisha ni kuwa iwapo Muhoozi angejaribu kuvaamia Kenya angechanganyikiwa kwa mazingira yake mazuri marefu, wanawake na mihadarati na hata kuporwa mjini Nairobi.

Video hiyo ilionyesha Omondi (akimwigiza Muhoozi) akijitokeza kwa helikopta akiwa amevalia mavazi kamili za kijeshi, akarukia Kenya.

"Namba moja, nambari moja tuko njiani kuvaamia Kenya," alisema.

Eric na  maafisa waliovalia kijeshi wakatazamakando kwa mshangao huku wakionekana kuchanganyikiwa kuhusu mahali walipotua.

Walikuwa wanatembea kwenye barabara kuu ya Nairobi ambapo Eric alikuwa anazungumza na mtu kwenye simu huku wakionyesha majumba makubwa yanayozunguka barabara ya Expressway, ambayo watu wengi wamelinganisha na Dubai.

Timu ya maafisa wa jeshi waliokuwa wamejihami kwa silaha wakatembea kando ya jumba ambapo walipigana na adui ambaye hakufichuka.

Waganda walimjibu huku wakimkejeli na kupakia picha zilizoashiria jinsi mchekeshaji huyo atakavyonyanyuliwa kupelekwa nchini Uganda kwa kuwachokoza.

Walieleza jinsi Omondi atasubiriwa kwenye Uwanja wa ndege wa Entebbe atakapo watembelea tena kwa minajili ya hafla za uchekeshaji.

"Kwa hivyo umeamua hutarudi nchini Uganda Eric?" Ismah aliuliza.

Hata hivyo, Wakenya walimpongeza kwa video hiyo na kwa kuzingatia masuala yanayotatiza Kenya na hata kujivunia jinsi Kenya ina majumba mazuri mazuri.

Eric Omondi amewashughulikia Waganda na Jenerali wao Muhoozi! Hio video ilikuwa ya kusisimua," Ramesh Saxena aliandika.