Nimeanza ku'unfollow watu wenye fikira mbaya - Willy Paul

Msanii huyo anachukua uamuzi huu siku chache baada ya kutupiwa maneno kwa kutoa 'rate card' yake.

Muhtasari

• Msanii huyo anachukua uamuzi huu siku chache baada ya kutupiwa maneno kwa kutoa 'rate card' yake.

Willy Paul aanzisha mchakato wa ku'unfollow wambea
Willy Paul aanzisha mchakato wa ku'unfollow wambea
Image: Instagram//WillyPaul

Msanii wa kizazi kipya nchini Kenya Willy Paul ametangaza kwamba ameanza mchakato wa kuafuta marafiki kwenye mtandao wa Instagram ambao wana roho mbaya na akili potovu.

Pozee alitangaza haya kupitia Instagram story yake ambapo alisema kwamba kama wewe ulikuwa rafiki yake na utaona ameku unfollow bas iujue ni miongoni mwa watu wale ambao amewaorodhesha kama wenye akili potovu kwake.

“Kwa hiyo leo nitakuwa nawa-unfollow watu wenye fikira potovu. Ikitokea nimeku-unfollow, tulia tu na ujikusanye na kuendelea na maisha yako…lakini bila mimi,” Willy Paul aliandika huku akimalizia kwa emoji za kucheka.

Haijulikani ni kwa nini msanii huyo ameamua kuchukua uamuzi huo ila baadhi wanahisi huenda ni wale waliotoa maoni hasi baada yake kuachia ‘rate card’ ambayo inaonesha jinsi atakuwa anatoza watu na makampuni yanayohitaji huduma zake za kutangaza biashara kwenye mitandao yake ya kijamii.

Siku chache zilizopita, Pozee aliachia tangazo hilo akisema kwamba yeyote anayemtaka kuonekana kwenye vklabu pasi na kufanya kitu chochote atahitaji kujihami na kitita cha laki 3 pesa za Kenya, huku kama unataka atumbuize kweney klabu hiyo basi sharti umpe laki 6 papo hapo pasi na ahadi.

Aliwashtua wengi aliposema pia kuwa kama unataka akuje kuzindua brand yako basi mtaanza mazungumzo kuanzia milioni 30 pesa za Kenya na hapa wakenya wengi waliongea maoni ya kila aina, mengi ambayo yalionekana kumkera.

“Kwa uchumi huu ni bora kusikiliza nyimbo zako wakati zimenyamazishwa” Shamsisomc aliandika.

Niko na kiulizo ,sasa wewe ukiitwa hizo doh utazileta ndio ulipwe hizo zako ,swali tu na nimekuja kwa Amani,” DJ Leen alimuuliza kwa kebehi.