Nisaidieni- Mcheshi Consumator akiri kumpenda msanii Justina Syokau

Anawaomba mashabiki wake kumsaidia kusambaza ujumbe huo hadi umfikie mwimbaji Justina.

Muhtasari
  • Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina Syokau,alifahamika sana  kwa wimbo wake wa 'Twendy Twendy'
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Mcheshi Peter Wamwea, ambaye hapo awali alikuwa mcheshi kwenye Churchill Show kwa jina la kisanii 'Consumator' ametangaza kumpenda mwimbaji Justina Syokau na kusema yuko tayari kumnunulia BMW X6 na hata kumvisha pete ya uchumba.

Anawaomba mashabiki wake kumsaidia kusambaza ujumbe huo hadi umfikie mwimbaji Justina.

Alinukuu akisema "Nisadieni imfikie Justina Syokau 2020"

Katika chapisho lake aliloweka kwenye Facebook alikuwa ameshikilia ubao uliokuwa na maandishi yaliyoandikwa,

"Justina Syokau, siwezi kukuficha hili tena. Nakupenda na nataka kukuoa, nataka kukuchumbia ndani ya BMW X6 nitakununulia. Nitakuozesha Zanzibar juu ya boti"

Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina Syokau,alifahamika sana  kwa wimbo wake wa 'Twendy Twendy'.

Kwa kweli Justina amekuwa akiwakosesha wanaume usingizi mitandaoni, swali lililosalia kwa mashabiki ni je msanii huyo atakubali ombi la mcheshi Consumator?

NISAIDIENI IMFIKIE Justina Syokau 2020

Posted by Consumator Comedian on Monday, November 14, 2022