'Nitakushika mkono daima,'Ujumbe mtamu wa Brenda Jons kwa dada yake

"Kwanza, heri ya kuzaliwa unapofikisha miaka 18 dada yangu...nimefurahi sana kukuona ukikua

Muhtasari
  • Mchekeshaji aliendelea kusema kuwa sasa hivi unakaribia kuanza mitihani yake na kwamba anamuombea Mungu anapojitayarisha
Brendah Jons
Image: Brendah Jons/INSTAGRAM

Mcheshi Brenda Jons ametumia ukurasa wake wa Instagram kusherehekea dadake siku yake ya kuzaliwa na pia kumtakia heri katika mitihani yake ijayo.

Alimtaja dada yake kama rafiki yake mkubwa na kwa ajili hiyo anampenda sana.

"Kwanza, heri ya kuzaliwa unapofikisha miaka 18 dada yangu...nimefurahi sana kukuona ukikua na kuwa msichana mzuri sana..nilikuahidi kukushika mkono daima na nitafanya...ata wewe unajua." sikuangushangi ."Ilisoma sehemu ya ujumbe wake.

Mchekeshaji aliendelea kusema kuwa sasa hivi unakaribia kuanza mitihani yake na kwamba anamuombea Mungu anapojitayarisha.

"Sasa hivi unakaribia kuanza mitihani yako kuu na nataka tu kukuombea ukiwa shuleni unapojiandaa na kusoma dakika za mwisho... Mola mwema akupe ukumbusho na ujasiri..umeyapata haya mama! All the best,"Aliandika Brenda.