Andrew Kibe: Nimewahi kuwa kinyozi, nikaosha magari, kuuza laini za simu

Hivi majuzi, Kibe alitangaza kununua gari aina ya Mercedes ambalo wataalam walidai linakwenda kwa takriban milioni 13 za Kenya.

Muhtasari

• "Nimeosha magari, nilijaribu kuwa fundi lakini yakaanguka. Nimeuza magari, nimeuza pikipiki..” Kibe alieezea.

Kibe Andrew
Kibe Andrew
Image: Instagram

Mwanablogu wa YouTube Andrew Kibe amesimulia jinsi alivyokwea ngazi za maisha kutoka alipokuwa hajulikani hata kidogo mpaka sasa hivi ambapo ni mmoja wa wanablogu YouTube wanaofagiliwa kwa kujijengea maudhui tofuati na wengine.

Kibe kupitia moja ya video yake YouTube, alieleza kuwa watu hawafai kumuona hivi sasa baada ya kununua gari aina ya Mercedes Benz na wafikirie alipata mteremko tu bali alipitia mambo mengi magumu ikiwemo kufanya baadhi ya kazi zisizo za stara.

Ama kwa hakika, hivi majuzi Kibe alijinunulia gari mpya kabisa aina ya Mercedes Benz $550 yenye thamani ya Milioni 13. Kulingana na ripoti, bei ya Mercedes $550 nchini Kenya ni kati ya KSh 8.65M hadi KSh 13.75M kutegemea muuzaji, maili, na mwaka wa utengenezaji.

Kibe alidai kuwa alipata gari la Mercedes Benz kutokana na mapato yake kwenye YouTube; na hata aliendelea kuwashukuru mashabiki kwa kumiminika kwenye chaneli yake ya YouTube ili kumwezesha kupata mapato aliyohitaji kupata gari hilo la kumezewa mate.

Akisimulia hayo hayo kupitia chaneli yake ya YouTube, Kibe alifichua kwamba aliwahi kufanya kazi kama kinyozi na mchuuzi pia miongoni mwa kazi zingine za kusaka tonge.

“Nimewahi lazimika kuuza sim-cards, nimekuwa kinyozi. Nimeuza sandwich nilipokuwa nikitazama raga. Nimeosha magari, nilijaribu kuwa fundi lakini yakaanguka. Nimeuza magari, nimeuza pikipiki..” Kibe alieezea.

Japo hakutaja, minong’ono ambayo imekuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu ni kwamba mwanablogu huyo kwa wakati mmoja aliwahi kuwa mhubiri wa kanisa ambapo alikuwa anawalisha waumini wa Mungu neon pasi na mchezo.