Corazon Kwamboka amuombea mwanamke aliyemfokea mitandaoni

Muhtasari
  • Kutoka kwa hadithi, alikuwa anazungumza juu ya "sisi" akimaanisha kuwa hakuwa akifanya peke yake
  • Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza kwa nini anazungumza "sisi" wakati aliachwa na  mpenzi wake
CORAZON KWAMBOKA
Image: HISANI

Kwa nini mtu achukue sehemu yako ya maoni au kujibu hadithi yako ikiwa ana jambo baya la kusema? Nadhani afadhali usitoe maoni yako.

Corazon Kwamboka alikuwa mwathirika wa aina hiyo. Alishiriki kwenye chapisho lake la Instagram jinsi shabiki alijibu kwa uchungu hadithi ambayo alikuwa ameshiriki.

Hadithi hiyo ilihusu jinsi walivyokuwa wakimfundisha bintiye Koko kulala. Pia alizungumzia jinsi ilivyomchukua Kiarie siku tatu kujifunza.

Kutoka kwa hadithi, alikuwa anazungumza juu ya "sisi" akimaanisha kuwa hakuwa akifanya peke yake.

Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza kwa nini anazungumza "sisi" wakati aliachwa na  mpenzi wake.

Corazon alijibu tu kwa ukomavu. Inaonekana hakuwa tayari kwa drama kati yake na shabiki huyo.

Aliposhiriki picha ya skrini ya mazungumzo yao, corazon aliwaomba mashabiki wake wamwombee mwanamke huyo.

Kulingana naye, mwanamke huyo hakuwa sawa na alihitaji sana maombi.

"Nahurumia watu kama hawa, yaani anakasirishwa na jinsi namfunza mtoto kulala,tafadhali muombeeni huyu dada kwani hayuko sawa," Kwamboka Aliandika.

Shabiki huyu alikuwa amemfokea Corazon jinsi ameachwa na wanaume.

"Unaongelesha nani, na 'sisi' ni akina nani uliachwa kila mwanamume uliyempenda anakuacha."

Katika mitandao ya kijamii asimia kubwa ya watu wanao wakejeli wanawake wenzao kwa hakika utaata ni wanawake pia.

Kweli hawakukosea waliposema adui ya mwanamke ni mwanamke mwenzake.