Samidoh asema mamake aliwahi mpa adhabu ya kulala ndani ya nyumba ya mbwa

Alisema mama yake alimfungia ndani ya nyumba ya mbwa kama adhabu ya kufika nyumbani kuchelewa.

Muhtasari

• Samidoh alisema alikuwa na tabia ya kufika nyumbani amechelewa alipokuwa mtoto mdogo, tabia iliyomchukiza mamake.

Samidoh, msanii na afande
Samidoh, msanii na afande
Image: Instagram//Samidoh

Msani maarufu wa nyimbo za Mugithi Samuel Michoki almaarufu kama Samidoh amewaacha mashabiki wake wakizungumza baada ya kukiri kuwa kuna siku mamake marehemu alimfungia ndani ya nyumba ya mbwa kama adhabu ya kuchelewa kufika nyumbani kama amechelewa.

Alisema mamake alikuwa mkali sana kwani kuna siku aliwahi kufika nyumbani saa saba za usiku baada ya kutoka kwa sherehe za mugithi za Mugithi Group Africa zilizokuwa zikifanyika eneo la Subukia lililoko kaunti ya Nakuru.

Siku hiyo aliporejea nyumbani alibisha nyumbani kwao na kufunguliwa na mamake, kisha kupakuliwa chakula na mamake. Alipoanza kula mama alimwamsha  babake aliyekuwa amelala saa hizo.

Baba Samidoh alipoamka, mamake aliwaambia wapigane ilikujua nani ndume wa nyumba na ni nani atakuwa anafika amechelewa kwa nyumba.

''Nataka kujua nani amenioa huku leo. Wacha kijana akule apate nguvu mpigane. Atakayeshinda huyo ndiye nitakuwa nafungulia mlango usiku wa manane.''  Samidoh aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Bila kusita wala kukawia baba yake alimrukia na kumcharaza makofi yaliyomfanya masikio yake kuwa mekundu. Alimwingiza chini ya meza na kumpiga mateke yasioisha.

Kwa huruma nyingi mama aliamua kumshika baba aliyekuwa amepandwa na mori kuwatenganisha.

''Babangu hakungojea niume kijiko ch tatu. Nilisikia nimepigwa makofi kadhaa pah! kabla ya kumaliza kusikia sauti ndani ya sikio! Nilikuwa chini ya meza nikitandikwa mateke.'' Samidoh aliendelea kusimulia.

Haikuishia pale, Mamake aliamua kumpa adhabu ingine kali ya kumtoa nje na kumfungia kwenye nyumba ndogo ya mbwa.

Adhabu ya mama ilimfanya kulia na kujuta kwa kulala kwenye nyumba ya mbwa hadi asubuhi. Alijaribu kumlilia mama amsamehe na hatarudia kosa la kufika nyumbani amechelewa ila mamake hakusikia ombi hilo.

''Mama tafadhari nifungulie nitakufa. Sitarudia''   Samidoh aliomba kwa upole.

Aliendelea na kusimulia na kusema, "Mamangu alinifungia akaenda kulala. Baridi niliihisi usiku wote. Kupe na Viroboto walikuwa wananiuma sana. Nilipiga kamsa nikiita Mama huku nikipiga ukuta wa nyumba hiyo ila hakuna aliyenisikia wala kunifungulia.''