Ukimtoa Diamond sisi wengine hatuna pesa - Gigy Money

Tunawadanganya tunavaa magauni ya milioni mbili na nusu ili mtuheshimu lakini kiukweli hakuna - Gigy Money.

Muhtasari

• Alitolea mfano wa wasanii wenzake Nigeria ambao wanazidi kufanya mambo makubwa kutokana na utajiri wa kweli wanaopata kimuziki.

Diamond na Gigy
Diamond na Gigy
Image: Instagram

Mwigizaji na msanii wa kike kutoka Tanzania Gigy Money ameibuka na masimango dhidi ya ndugu zake walioko kwenye Sanaa ya Tanzania kuwa ni maskini wa kutupwa wala pesa.

Money ambaye alikuwa akizungumza moja kwa moja kwenye Instagram yake alisema kwamba wasanii wa Tanzania wanashobokea mambo tu na kujionesha mitandaoni kwa vitu ambavyo wamekodi ili kupiga picha navyo kuonekana wana mali ya kifahari kumbe hali halisi ni maskini hohe hahe.

Mwigizaji huyo ambaye pia ni mwanafasheni alisema ukimtoa msanii nguli kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz, basi wengine wote ni rundo moja la wale wasiokuwa na mihela kabisa.

Ukimuondoa Diamond Platnumz, wasanii wa Tanzania wengine tunaobaki hatuna pesa, tunawadanganya tunavaa magauni ya milioni mbili na nusu ili mtuheshimu lakini kiukweli hakuna wa kuvaa nguo ya milioni mbili kwa wasanii wa Tanzania" Gigy Money alisema.

Alitolea mfano kuwa wasanii wenzao kutoka Nigeria wana mihela mingi na ndio maana wanakatiza ndani ya magari mazuri, mavazi ya kishua na mijengo ya kutamanika kutokana na utajiri wao mwingi wanaovuna kutokana na miziki ya Afropop.

“Kama unaona huyu Ruger, kama unaona huyu Kizz Daniel wanajenga vitu kila siku, lakini na sisi ni Mungu tu anajua. Adhabu tunayopata huku ni kutumbuiza kwa shilingi milioni moja za Kitanzania, hiyo ni nini sasa,” Gigy Money aliuliza.

msanii huyo mwenye utata anazungumza haya siku chache tu baada ya msanii Harmonize kuimba kwenye collabo na Kontawa akisema kwamab ametoka nyuma na kuwa na mafanikio makubwa kuliko Diamond Platnumz pamoja na mameneja wote wa lebo ya WCB Wasafi.