DJ Mo amwandikia mwanawe ujumbe mtamu anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

"Siku kama hii miaka 7 iliyopita nilikua baba kwa mara ya kwanza.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ujumbe wake Mo amekumbuka jinsi mwanawe alibadilisha maishaa yake baada ya kuzaliwa miaka 7 iliyopita
Muraya-ladasha-size-8-mpasho
Muraya-ladasha-size-8-mpasho

Mcheza Santuri maarufu DJ Mo amemnakilia kifungua mimba wake Ladasha ujumbe wa kipekee, siku hii anaposherekea siku yake ya kuzaliwaa.

Kupitia kwenye ujumbe wake Mo amekumbuka jinsi mwanawe alibadilisha maishaa yake baada ya kuzaliwa miaka 7 iliyopita.

Ladasha Wambo ni kifungua mimba wake DJ Mo na msanii wa nyibo za injili Size 8.

Mo alimwombea mwanawe ulinzi wake Mungu huku akikiri hamna kitu ambacho kitawatenganisha,na kuingilia upendo wao.

"Siku kama hii miaka 7 iliyopita nilikua baba kwa mara ya kwanza. Mtoto wa kike alizaliwa na maisha yangu yakabadilika. Wambo , Umetamani kuwa na miaka 7 na leo Mungu amefanikisha 😍🥰. @ladashabelle.wambo , Unajua jinsi ninavyokupenda , na nakuombea kwa Mungu akulinde daima , akuongoze na kukupa Fadhila . Hakuna kitakachokuja kati yetu."

Kwa upande mwingine msanii Size 8 alissema;

"Ni furaha iliyoje siku hii..... Binti yangu anatimiza miaka 7 😍❤️ happy birthday @ladashabelle.wambo.... Mungu amekuwa mwaminifu kweli mummy😍 💋❤️......."