Aliyekuwa mpenzi wa Harmonize afunga harusi na mume tajiri

Wolper alikuwa mchumba wa kwanza wa msanii Harmonize akichipukia na walitengana mwaka 2017.

Muhtasari

โ€ข Kiapo hiko jamani cha Milele๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘ŒMungu akatende Na ikawe Milele kabisa Bila kikwazo Tunashukuru Akukua na pingamizi - Wolper.

Wolper afunga ndoa na mume mpya
Wolper afunga ndoa na mume mpya
Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe wa Bongo Fleva na ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mpenzi wa kwanza kabisa wa msanii Harmonize enzi anachipukia, Jacqueline Wolper hatimaye ameiaga soko ya kutafuta mpenzi.

Hii ni baada ya kufunga harusi na mpenzi wake wa muda mrefu, mfjasiriamali Rich Mitindo katika kanisa moja nchini Tanzania.

Harusi hiyo ambayo ilizungumziwa sana mitandaoni wikendi iliyopita na Wolper ambaye wengi wanamjua kama Mama P alionesha kufurahishwa kwake kupitia Instagram yake.

"Huu wakati tu๐Ÿ˜Œโค๏ธโค๏ธโค๏ธ Moyo wa shukurani ๐Ÿ™Wapenzi hivi karibuni tunaingia mubashara @bona_tv." Wolper alinukuu picha zilizopigwa wakati wa harusi hiyo.

Wanandoa hao walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja, mtoto wa kiume, mwaka jana.

Wolper na Mitindo walianza kuchumbiana mwaka 2016 ambapo walikutana tu kama wafanyibiashara wa kushirikiana na katika safari hiyo mapenzi yakazaliwa.

โ€œKisha tungekutana kwenye tamasha la biashara wakati sisi sote wawili tulikuwa single mnamo 2020, tuliishi kwa upendo na Mungu alitubariki na mtoto. Naomba upendo na heshima uliyonipa ibaki milele na milele,โ€ Wolper aliandika hivi karibuni.

โ€œSiwezi kueleza furaha yangu lakini hii ni siku nzuri sana ambayo sitaisahau kamwe. Katika maisha yangu sijawahi kupata upendo na furaha kama hii. Ilikuwa ndoto yangu kuwa na familia lakini sasa wakati ni sasa. Kwa hili nakuthamini sana Jacq wangu na nitampenda sana mwanangu maana umembeba ndani yako. Ninaahidi kuwa baba mzuri na mshirika mwaminifu katika siku zote tutakazokuwa pamoja.โ€ Rich Mitindo alimuandikia kipindi hicho wanatarajia mwanao.

Kabla ya kuanza kuchumbiana na Rich, Wolper alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Konde Music Worldwide Harmonize na baada ya kuachana mwaka 2017.

Baada ya kula kiapo kanisani, Wolper alisema kuwa anaomba sana iwe kheri na furaha ya milele maishani mwao.

โ€œKiapo hiko jamani cha Milele๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘ŒMungu akatende Na ikawe Milele kabisa Bila kikwazo Tunashukuru Akukua na pingamizi Maana Nasikiaga Mapingamizi yanaibukaga Tuu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Nipende kutoa shukurani kwa kanisa letu Takatifu sentpeter Father na Ma kateksta wote Na masister wote Tunashukuru sana Na Mungu akazidi kuwainua watumishi wa Mungu Mzidi kututumikia kama ilivyoandikwa na Tutawaheshim sana Mungu awabariki sana,โ€ aliandika.