Hii ni ndoto ambayo niliombea - Nana Owiti asema akionesha familia yake

Aliwashauri watu kutokata tamaa na kuondoka kweney uhusiano pindi changamoto kidogo zinapobisha.

Muhtasari

• Aliwashauri watu kutochoka haraka katika uhusiano pindi changamoto kidogo zinapobisha.

• Tusiwe wepesi wa kukimbia kwa ishara ya kwanza ya kutishia uhusiano. Hakika ni barabara yenye alama nyingi sana - Owiti alisema.

Nana Owiti asema familia yake ni ndoto ambayo aliiombea muda mrefu
Nana Owiti asema familia yake ni ndoto ambayo aliiombea muda mrefu
Image: Instagram

Mwanahabari Nana Owiti ameonesha familia yake yote kweney mitandao ya kijamii na kusema kwamba kwa muda mrefu alikuwa anamuomba Mungu kumjaalia familia kama hiyo, naye Mungu asiye mchoyo akampa zaidi ya kile alichokuwa akikiomba enzi za ujana wake.

Owiti kupitia ukurasa wake wa Inatagram alisema kuwa anajihisi mwenye faraja kubwa kupata uzoefu wa moja kwa moja kuwa mama wa familia na mke wa msanii mkubwa mwenye ushawishi wa aina yake, King Kaka.

“Hili halikuwa lengo tu bali ndoto. Niliota hii na niliiombea. Nimebarikiwa kuiona. Mara nyingi, watu wataonyesha jinsi tulivyo bora..Wengine watauliza jinsi tulivyoifanya..lakini hakika ninakuambia…Mnachokiona hapa ni bidhaa ya mwisho. Usizingatie hilo. Imekuwa kazi safi nyuma ya pazia,” Owiti aliandika.

Pia alifichua kuwa wengi wanafikiri kuikuza familia ni kitu rahisi lakini akakanusha na kusema kuwa imekuwa safari ndefu yenye milima na mabonde, machozi na furaha gharika na nyika bila kusahau magumu yote ambayo yamewakumba kama wanadamu wengine.

 Owitibaliwashauri watu kuwa ukitaka kitu king’ae lazima uwe tayari kuvumilia muda hakijatakata. Aliwaambia kuwa ni vizuri watu kuwa na uvumilivu wa kukabili mambo badala ya kuyakwepa kwa kutoroka kwani hata dhahabu kabla kutokea na urembo wake wote, sharti mwanzo ipitishwe katika tanuru la moto.

“Imekuwa damu, jasho na machozi mengi. Imekuwa mizigo na maombi mengi lakini ambayo labda hautayaona. Kama kizazi, tusizingatie sana bidhaa ya mwisho. Wacha tuingie kwenye uhusiano tukijua itachukua mengi. Tusiwe wepesi wa kukimbia kwa ishara ya kwanza ya kutishia uhusiano. Hakika ni barabara yenye alama nyingi sana. Tusikate tamaa mapema sana 🙏” Nana Owiti.