Jux anyoosha maelezo kuhusu kutoka kimapenzi na Paula Kajala

Msanii huyo tangu kuachana na Vanessa Mdee, amekuwa akiweka maisha yake ya kimapenzi nyuma ya pazia kiasi kwamab hakuna anayejua anachumbiana na nani.

Muhtasari

• Nadhani ni kwa sababu aliwahi kupost akiimba wimbo wangu ‘Kiss’ na alikuwa anavaa collection yangu ya African boy - Jux.

Juma Jux azungumzia ishu ya kuchumbiana na Paula
Juma Jux azungumzia ishu ya kuchumbiana na Paula
Image: Instagram

Mwanamuziki wa RnB kutoka Tanzania Juma Jux ameamua kunyoosha maelezo kuhusu kile kinachodhaniwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi baina yake na mfanyibiashara wa nguo chipukizi, Paula Kajala ambaye ni mtoto wa mwigizaji mkongwe Kajala Masanja.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Wasafi Media, Jux alisema kuwa uhusiano wake na kijana huyo wa kambo wa msanii Harmonize ni wa kibiashara tu na wala hawajawahi kuvuka mipaka kuingia kimapenzi hata mara moja.

Msanii huyo aliwekwa kwenye kiti moto na kulazimika kuitetea video ambayo ilidaiwa kuwa Paula alionekana akiingia kwenye nyumba yake ila akakanusha madai hayo na kusema kuwa hata hajawahi fika katika makazi yake.

Alisisitiza kwa kumtaja Paula kama dadake mdogo tu na wala hawezi kuingiwa na suala la kumtongoza au kumuomba kuwa wapenzi, huku akisema yeye yupo kwenye uhusiano mwingine ambao unampa Amani ya akili kupita maelezo.

"Hapana, ninachoweza kusema ni kama dada yangu mdogo. Hajawahi kuja nyumbani kwangu. Sijawahi kuona hiyo klip. Ndio, kwenye klipu, inaonekana kama nyumba yangu. Sikumbuki ni muda gani nilimuona. Ukweli ni kwamba, yeye ni msichana mdogo ambaye namuona akifanya mambo yake. Hatuko kwenye uhusiano kwa sababu niko kwenye uhusiano wangu mwenyewe,” alisema.

Mdanii huyo mwenye sauti nzuri ya kusifiwa na wanawake pamoja pia na mitindo yake ya kuvaa alikisia kuwa huenda watu walianza kumhusisha kuwa kimapenzi na Paula baada ya kuonekana akifanya challenge ya wimbo wake mpya wa Kiss Ambao amewashirikisha magwiji wa Amapiano kama kina Marioo.

 “Nadhani ni kwa sababu aliwahi kupost akiimba wimbo wangu ‘Kiss’ na alikuwa anavaa collection yangu ya African boy. Sijui kwanini anahusishwa na mimi."

Rayvanny baada ya kusemekana kuwa kweney uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Rayvanny, hivi karibuni mwanamuziki huyo aliweka wazi kwamab alilazimika kukatisha uhusiano wake na binti huyo wa Kajala kutokana na mambo mengi kupishana baina yao.

Kwa upande wa Jux, tangu kubwagwa na mwanamuziki na pia aliyekuwa mtangazaji Vanessa Mdee, amekuwa akiweka maisha yake ya kimapenzi nyuma ya pazia sana kiasi kwamba hakuna anayejua anachumbiana na nani.

Vanessa Mdee alitimkia Marekani na kuolewa na mwanamuziki Rotimi ambaye hivi majuzi wametangaza kutarajia mtoto wa pili pamoja.