Nameless: Ndoa yetu si 'perfect' hata sisi hupigana, hatukubaliani kwa kila kitu

Nameless alikuwa anamjibu shabiki mmoja aliyetaka kujua kama wao hukosana na mke wake Wahu.

Muhtasari

• Wawili hao wamedumu kwenye uhusiano kwa zaidi ya miaka 25, 17 kati yao ikiwa ni halali kabisa katika ndoa.

Nameless asdhibitisha kuwa ndoa yao pia si kamilifu
Nameless asdhibitisha kuwa ndoa yao pia si kamilifu
Image: Instagram

Msanii mkongwe wa Kenya Nameless amedhibitisha kuwa ndoa yake na mke wake ambaye pia ni mwanamuziki Wahu Kagwi si dhabiti sana kama ambavyo wengi wanavyoichukulia na kuwasifia mitandaoni.

Nameless alifichua kwamba hata wao wakati mwingine hukosana na hata kupigana lakini kwa heshima tu. Alisema kuwa katika ndoa, kupishana maelewano na kukasirikiana kwa muda ni jambo la kawaida hata kama mashabiki wao wengi huwaona kama wanandoa waliotimilika katika kila kitu.

Alikuwa anamjibu shabiki mmoja aliyewapongeza katika picha yake ya Facebook akiwa pamoja na mpenzi wake Wahu na shabiki huyo aliwaambia wako sawa ila akataka kujua iwapo wao huvurugana nyumbani.

“Mko sawa, nyinyi watu hupigana kweli kwa sababu mapenzi yenu ni moto kila siku,” shabiki kwa jina Milkah Wilson aliuliza kwa umakini mkubwa.

Nameless alijibu kuwa wao kwa kweli hupigana lakini kiheshima na kuwa kila siku kwao ni nafasi nyingine ya kujifunza jinsi ya kuishi maisha mazuri, kinyume na dhana iliyoko vichwani mwa wengi kuwa wawili hao hawajawahi kukosana katika ndoa.

“Tunapigana kwa uhakika. Lakini tunafanya kwa heshima nadhani.. na tunajaribu kutatua haraka.. hatukubaliani kwa kila kitu. Tunajifunza kila siku kuishi bora na kila mmoja. Kwa sababu sisi sote tunataka furaha na amani ya akili,” Nameless alijibu.

Nameless na Wahu wamedumu kwenye mahusiano kwa jumla ya miaka 25, miaka 17 kati yao ikiwa halali kabisa kweney ndoa.

Katika siku ya kusherehekea miaka 17 ya ndoa yao, Wahu alifichua kwamba kuna jarida moja maarufu lililokuwa humu nchini kipindi wanafunga harusi yao na lilitabiri kuwa naingedumu zaidi ya miaka miwili, aliwasuta kuwa miaka 17 baadae bado ndoa yao imegandiana kwa pamoja kama ruba.

Wanandoa hao hivi karibuni walimkaribisha mtoto wao wa tatu ambaye nib inti na wanajivunia kuwa wazazi walezi wa mabinti.