Tuongeze mapacha! BillNass amjibu Nandy baada ya kusema anataka mtoto mwingine

Nandy alikuwa amemwambia mumewe kuwa anataka kuongeza mtoto mwengine

Muhtasari

• Nandy aliweka picha akiwa na mume wake wakiwa wameshikana mikono.

Billnass na Nandy
Image: Nandy Instagram

Mumewe mwanamuziki wa Tanzania Nandy, BillNass amemjibu mke wake kuhusiana na suala la kupata mtoto mwengine ambalo amekuwa akisisitiza mtandaoni.

Kwenye Instagram, Jumanne, mwanamuziki Nandy alizua gumzo mtandoni baada ya kumwambia mume wake BillNass kuwa anataka mtoto mwengine kwa mara ya pili.

Nandy aliweka picha akiwa na mume wake huku wakiwa wameshikana mikono na kusema anachohitaji na ambacho kimekuwa kikimkwaza.

"MUME WANGU ❤️! @billnass ETI TUONGEZE MWINGINE," Nandy alisema.

Nas alikubaliana naye na kumwambia kuwa wanaweza kujaribu kuzama kwenye matukio ya kumleta mtoto mwingine duniani kwani hata yeye ana hamu ya kuwa mzazi kwa mara nyingine tena.

"Sio mwingine tu, tuongeze wengine tafadhali ikiwezekana Mapacha ❤️ Nimechoka Kumngángánia Huyu Mmoja @officialnandy," BillNass alimjibu mpenzi wake.

Hivi majuzi, mwanamuziki huyo aligusia suala la kuongeza watoto alipopakia picha ya mume wake akijivinjari kwa kupepea juu ya bahari na parachute.

Nandy kwa mzaha, alionekana kumtahadharisha Billnass kutoshiriki katika mchezo kama huo hatari ambao huenda parachuti ile ikifeli atazama kwenye bahari hiyo kama bado hajampa mapacha.

Alimwambia kwamba licha ya kuhangaika kujipa raha kwa kupepea kwa chombo hicho lakini anafaa kuweka kichwani mwake kwamba ana deni kubwa kwa mkewe Nandy ambalo ni sharti alitimize – deni la kumzalisha watoto mapacha!

Unajua bado hujanipa mapacha eeeeeee!!!!! We hangaika tu!!!! Sema nimetamani..😋😋 @billnass,” Nandy alimtania huku mwisho akisema kuwa hata yeye ametamani kushiriki mchezo ule wa kujiburudisha kwa parachuti angani.