Guardian Angel amsifia Musila, asema ni 'crush' wake wa milele

Mwenyekiti huyo wa injili Kenya alisema kuwa Musila ni mmoja wa watu ambao hawezi kutafakari maisha bila wao.

Muhtasari

• Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa takribani mwaka mmoja tangu kufunga ndoa yao ya faragha mnamo Januari mwaka huu.

Guardian Angel amsifia mkewe Musila
Guardian Angel amsifia mkewe Musila
Image: Instagram

Mwimbaji wa injili Guradian Angel amemsherehekea mkewe Easther Musila kwa njia maalum baada ya kupakia picha yake na kusema kuwa kila anapomtazama tu huona kile ambacho Mungu amemfanyia katika maisha yake.

Mwenyekiti huyo wa injili Kenya alisema kuwa Musila ni mmoja wa watu ambao hawezi kutafakari maisha bila wao na kuchagiza kuwa ni ‘crush’ wake wa muda wote.

“Kile ambacho Mungu amenifanyia, huyu ndiye crush wangu wa milele,” Guardian Angel aliandika Instagram.

“Supastaa wangu,” Musila alijibu.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa takribani mwaka mmoja tangu kufunga ndoa yao ya faragha mnamo Januari mwaka huu.

Ndoa yao iligonga vyombo vya habari na mablogu Afrika Mashariki kutokana na kwamba Guradian Angel ni mdogo zaidi kiumri kulinganishwa na Musila.

Guardian Angel ana miaka 31 huku Musila mkewe akiwa na miaka 53, tofauti ya miaka ishirini na ushee kati ya wapenzi hao.

Hivi majuzi mwanamuziki huyo alimsifia Musila na kusema kwamba tangu wajuane ameona mafanikio makubwa pamoja na mabadiliko katika maisha yake. Angel alisema kuwa ameanza kupata mapato ya haiba yake kutokana na muziki wake tangu aanze kuchumbiana na Musila ambaye amembadilisha na kumpa utulivu wa kiakili kusababisha kufanay muziki mzuri.

Guardian Angel na Esther Musila walipatana mwaka jana kupitia tafrija iliyowaunganisha na mtangazaji maarufu wa redio nchini, Maina Kageni.