Jacque Maribe: Kumlea mtoto Zahari ni raha sana

Maribe alisema kuwa mwanawe Zahari muda wote humpa fahari ya kuwa mama.

Muhtasari

• Maribe aliandika jinsi mtoto wake amekuwa mchangamfu na anayefahamu mambo mengi yanayomshangaza.

• Alisema kuwa yeye humtuza Zahari anapofanya vyema kwenye masomo yake

Jacque Maribe na Zahari
Image: Maribe Instagram

Aliyekuwa mwanahabari Jacque Maribe amemsherehekea mwanawe kwa picha anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kwenye Instastory zake, Maribe alilinganisha picha za mwanawe alivyokuwa mdogo na sasa ambapo amefikisha miaka 8.

Aliandika jinsi mtoto wake amekuwa mchangamfu na anayefahamu mambo mengi yanayomshangaza.

"Ilivyoanza, Zahari May 2014," Maribe aliandika.

"Inavyoendelea, Zahari Novemba 2022," aliandika huku akipakia picha yao ya sasa.

Alieleza jinsi alivyofurahi kumlea mwanawe ambaye sasa hivi amekuwa kijana mkubwa kidogo.

"Kumlea Zee. Alichagua filter ya cartoon. Mimi niko tu wueeh! Halafu mwanangu hapa ananiambia kuwa anataka kupaka nywele zake rangi sasa ambapo shule zimefungwa, kabla nionyeshe mshtuko wangu rangi aliyochagua ilinimaliza," Maribe aliandika.

Aliendelea kueleza kuwa mwanawe amekuwa mtiifu na mwenye bidii kwa masomo yake kwani amefaulu kwenye mitihani yake.

Alieleza jisi alivyomuahidi mtoto wake kumtuza likizo iwapo atapita kwenye mitihani yake.

"Mazungumzo na Zee wakati wa likizo..

Zee: Mama ulisema kuwa nikipata alama nzuri kwenye mitihani yangu utanipeleka mahali popote.

Mimi: Nikikumbuka kuwa ilikuwa manaeno matamu ya kumfanya afanye bidii kisha huyo akaniletea alama zote za A.

Zee: Nataka kuenda ulikoenda huko Italy, na kulikuwa na bahari, tunaweza kuenda huko?

Mimi: Nikapigia benki kuangalia fuliza

Zee: Au mama nipeleke nitazame World Cup

Mimi: Qatar kumejaa

Zee:Ah basi tuzuru nchi unayotaka wewe.

Mimi: Nikafikiria, Uganda ni hapa tu," Maribe aliandika.

Hivi majuzi, aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill, Eric Omondi alifichua kuwa yeye na anayedaiwa kuwa mzazi mwenzake ,Jacque Maribe, wana uhusiano wa karibu.

Katika mahojiano na Mwende Macharia, Omondi alisema kuwa yeye huwasiliana mtoto wa Maribe na kumjulia hali mara kwa mara.

Pia alisema yeye na Maribe huwasiliana anapokuwa akizungumza na mtoto Zahari na kuweka wazi kuwa wana urafiki wa karibu.