Bahati adokeza kufunga pingu za maisha hivi karibuni

"30TH NOVEMBER 2022 🌹 ❀ πŸ’," aliandika.

Muhtasari

β€’ Baadhi ya mashabiki wake wameachwa wakikisia kuwa anapanga kufunga pingu za maisha na Diana mnamo siku hiyo. 

β€’Alisema sababu yake ya kukawia kufanya harusi ni kwa kuwa anapanga harusi kubwa ya kifahari

Bahati na Diana Marua

Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati amezua gumzo mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe unaoashiria kama kwamba anapanga kufanya harusi hivi karibuni.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati alipakia picha ya ua lenye pete. Juu ya picha hiyo kulikuwa na maandishi mekundu ya tarehe  'Novemba 30.'

"30TH NOVEMBER 2022 🌹 ❀ πŸ’," aliandika chini ya picha hiyo.

Hata hivyo, mchumba huyo wa Diana Marua wanne hakutoa maelezo zaidi kuhusu ni nini haswa kitakachofanyika mnamo tarehe hiyo. 

Baadhi ya mashabiki wake wameachwa wakikisia kuwa anapanga kufunga pingu za maisha na Diana mnamo siku hiyo. 

Wengine hata hivyo waliamini kuwa anapanga kuachia wimbo mpya huku wengine wakimpongeza kwa mafanikio wasiofahamu.

"Unafunga ndoa au mimi ndio sielewi πŸ˜†,"vexivilla alisema.

"Baha ni siku ya kuzaliwa ama ni harusi?" monicaauma49 alihoji.

"HONGERA .πŸ‘πŸ‘πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯," aliandika imeld_amutabuzi .

"BAHA UMEANZA HAMASISHO NA HUU UCHUMI 😍😒😒😒😒πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ™Œ,"nella.e.h_h alisema.

Hivi majuzi, wakati wa hafla ya kufichua jinsia ya mtoto wao mchanga, Bahati alifunguka kuhusu sababu ya kukawia kufanya harusi.

Alisema sababu yake ya kukawia kufanya harusi ni kwa kuwa anapanga harusi kubwa ya kifahari na hangetaka kufanya harusi ndogo.

Aidha, mwimbaji huyo kijana alifichua kuwa atafunga pingu za maisha na mkewe Diana Marua hivi karibuni.

Ni wazi kuwa Bahati ni mwanamume anayependa kumzawadi mkewe kwa vitu vya thamani na vya kifahari kama vile nyumba,magari na vito mbali mbali.

Wapenzi hao hukabidhiana zawadi haswa katika siku maalum kwao.