(+VIDEO)Natamani Papa Shirandula angekuwa aone haya yakitimia- Jalang'o

Mbunge huyo amekumbuka akimwambia marehemu Papa Shirandula kuhusu kutaka kuitwa mhesh.

Muhtasari
  • Jalango aliandika ujumbe mtamu kwa marehemu Papa Shirandula, na tukio alipokuwa akiigiza kwenye kipindi cha Papa Shirandula
Jalango
Jalango
Image: Hisani

Mbunge wa Lang'ata Felix Odiuor almaarufu Jalang'o kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter ametamani Papa Sharandula angekuwa hai ili kushuhudia mafanikio yake.

Mbunge huyo amekumbuka akimwambia marehemu Papa Shirandula kuhusu kutaka kuitwa mhesh.

Jalango aliandika ujumbe mtamu kwa marehemu Papa Shirandula, na tukio alipokuwa akiigiza kwenye kipindi cha Papa Shirandula.

"Kwa wakati wa Mungu!! Natamani papa angekuwa hapa aone haya yakitimia!'

Katika klipu hiyo ya sekunde 26, mhusika Jalango anamwambia Papa kwamba sasa atatajwa kwa jina maalum.

"Mimi wamebadilisha mambo mengi hata jina yangu siku yangu kwanza kuniiita othesh othesh, hapana kabla hujafikia jina langu utapitia kitu inaitwa title, honorable, minister, prime minister, his excellency "

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 58 alifariki mwaka 2020 kufuatia matatizo ya kupumua alipokuwa akisubiri matibabu katika hospitali kuu ya kibinafsi.