Wewe ni mwamba katika tufani ,'Julie Gichuru amwambia mumewe huku wakisherehekea miaka 19 kwenye ndoa

Julie alimlimbikizia mumewe sifa,huku akitaja kuwa mwamba wake wa maishani.

Muhtasari
  • Wawili hao ni miongoni mwa wanandoa maarufu wa kupigiwa mfano mwema, na ambao wamekaa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10
JULIE GICHURU NA MUMEWE ANTHONY
Image: KWA HISANI

Mwanahabari Julie Gichuru kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesherehekea miaka 19 kwenye ndoa, na miaka 23 akiwa pamoja na mumewe.

Julie alimlimbikizia mumewe sifa,huku akitaja kuwa mwamba wake wa maishani.

Wawili hao ni miongoni mwa wanandoa maarufu wa kupigiwa mfano mwema, na ambao wamekaa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10.

Pia alimshukuru Mungu kwa kumleta mumewe maishani mwake, amemuahidi kumpenda milele.

"Happy anniversary mpenzi wangu ❤️ Miaka 19 ya ndoa, miaka 23 pamoja ❤️❤️ Najisikia kama jana simba wangu wa thamani! Ninamshukuru Bwana kwa kunipenda sana hata akatuleta pamoja! Ninakupenda kabisa, kabisa, bila kubatilishwa - sasa na hata milele."

Aliendelea;

Wewe ni mwamba, kimbilio katika tufani; Imani yako ni Nyota ya Kaskazini - mwongozo, mwanga, nguvu zetu; bidii yako na nidhamu ya ajabu ni msukumo  na wema wako ndio mlango wa neema ya Mungu katika maisha yetu ❤️❤️❤️🤗🙏

Asante Bwana, Mungu Mwenyezi Asante Anthony, kwa kunipenda ❤️❤️❤️ happy anniversary  kipenzi changu, mpendwa wangu, simba wangu, Mfalme wangu!."